NIMEFUNGUA MILANGO-RAS TABORA
RAS mpya wa Mkoa wa Tabora ndugu Msalika Makungu aanza kazi rasmi kwa kufanya ziara katika Wilaya za Tabora ambapo jana alikuwa katika Wilaya ya Sikonge. Alipata fursa ya kuhudhuria Baraza la Madiwani lakini pia alizungumza na watumishi wa Halmashauri.
Ziara hiyo ilikuwa na malengo ya kuifahamu jografia ya Mkoa wa Tabora lakini pia kufahamiana na viongozi pamoja na watumishi atakaofanyanao kazi katika Wilaya za Mkoa huu. “Mimi ni muumini wa uongozi wa pamoja, mimi ni muumini wa kutumikia majukumu na sio kutumikia cheo. Kwahiyo nimefungua milango katika sekretarieti yangu kuhakikisha kuwa nawatumikia wananchi…” alisema hayo RAS akizungumza na Baraza.
Aidha, Makungu alisisitiza juu ya kushirikiana katika uongozi wa pamoja ili kuwatumikia wananchi ambao mwaka 2015 waliamini na kupiga kura ya kutaka mabadiliko hivyo mabadiliko lazima wayaone katika vitendo vyetu na huduma wanazozipata kutoka kwetu.
Pia alizungumzia tatizo la utoro na mimba za utotoni kwa wanafunzi ambalo limekuwa ni tatizo la muda mrefu kwa Mkoa wa Tabora. Pamoja na hilo aligusia uchumi wa viwanda kama sera ya Serikali ya awamu ya tano inavyosisitiza jambo hilo, ni kuwataka kuungana pamoja ili kutekeleza maagizo ya Serikali hii na kutatua matatizo yanayoikabili Nchi yetu.
Aidha, Waheshimiwa Madiwani wakiongozwa na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge, Mhe. Peter Nzalalila, walifurahi sana kwa kujumuika na RAS katika kikao cha Baraza la Madiwani na kuahidi kuwa watakuwa bega kwa bega katika kuwatumikia wananchi na kuleta maendele ya Nchi yetu kwa ujumla.
Mkurugenzi Mtendaji Sikonge DC
Anuani ya Posta: S.L.P 70 Sikonge, Tabora
Simu: 0767135460
Simu: 0767135460
Barua pepe: ded@sikongedc.go.tz
Hatimiliki ©2017Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge, Haki zote zimehifadhiwa