Ofisi ya mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Sikonge imeendesha mafunzo kwa watumishi wa umma wa ajira mpya waliopangiwa kazi wilaya ya Sikonge.
Akifungua mafunzo hayo ya siku moja Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Sikonge Ndg. Seleman Pandawe amewaasa watumishi hao kuzingatia kanuni na maadili ya utumishi wa umma wakati wote wa maisha yao ya utumishi ndani na nje muda wa saa za kazi na kuhakikisha wanatoa huduma bora na kwa wakati kwa wananchi wa Sikonge.
“Wekeni malengo,toeni huduma bora kwa wananchi bila upendeleo,zingatieni sheria na haki katika utoaji wa huduma.Jengeni mahusiano mazuri mahala pa kazi na kuwa watiifi kwa serikali iliyopo madarakani.”Ameeleza Ndg. Pandawe.
Kw upande wake Katibu Tawala wilaya ya Sikonge Ndg. Andrea Ng’hwani amewapongeza watumishi hao kwa kupata nafasi ya kuajiriwa na kuwataka kufuata kanuni za utumishi na kuwa na moyo wa kujifunza wakati wote wanapokuwa watumishi wa umma na kuwa mstari wa mbele katika kusukuma gurudumu la maendeleo ya wilaya ya Sikonge.
Mkuu wa divisheni ya Utawala na usimamizi wa rasilimali watu Ndg. Nico Kayange amewasisitiza watumishi hao kuzingatia utunzaji wa siri za serikali na kufuata sheria za utumishi wa umma kwa kuepuka kuwa wasemaji wa mambo ya serikali.
Naye mkuu wa divisheni ya elimu sekondari Bi. Kalista Maina amewaeleza watumishi hao wa ajira mpya hajawahi kutamani kuhama Sikonge kwa jinsi Sikonge ilivyo sehemu salama kwa utumishi waumma na kuwasihi kuwa na ushirikiano katika kutekeleza majukumu yao ya kila siku.
Mafunzo hayo yamejumuisha watumishi wa ajira mpya toka kada mbalimbali wakiwemo watendaji wa vijiji,watunza kumbukumbu,waandishi waendesha ofisi,maafisa ustawi wa jamii,maafisa habari,madereva,mkaguzi wa ndani, Afisa maendeleo ya jamii pamoja na watoa mada kutoka ofisi ya TALGWU mkoa wa Tabora na mwakilishi toka ofisi ya mfuko wa hifadhi ya jamii wa PSSSF mkoa wa Tabora. Mafunzo haya ni hatua muhimu katika kuhakikisha watumishi wanakuwa na uelewa mzuri wa majukumu yao na kuweza kutoa huduma bora kwa wananchi wa Sikonge.
Mkurugenzi Mtendaji Sikonge DC
Anuani ya Posta: S.L.P 70 Sikonge, Tabora
Simu: 0767135460
Simu: 0767135460
Barua pepe: ded@sikongedc.go.tz
Hatimiliki ©2017Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge, Haki zote zimehifadhiwa