Na. Robert Magaka ,Sikonge – Tabora.
Kauli hiyo imetolewa leo na Mkuu wa Wilaya ya Sikonge Mhe. Simon Chacha alipokuwa akihutubia wananchi waliohudhuria maadhimisho ya Siku ya Ukimwi Duniani yaliyofanyika katika Ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge.
Aidha Mhe. Chacha amewasihi wananchi kuitikia wito wa kauli mbiu ya Siku ya Ukimwi duniani unaosema “Jamii iongoze kutokomeza Ukimwi” kwa kujitokeza kwa hiyari kupima virusi vya Ukimwi na kuanza kutumia dawa mapema kwa wale watakao bainika kuwa na maambukizi.
Akitoa Salamu za Chama, Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Sikonge Bi. Anna Chambala ameutaka umma kuendelea kuongoza mapambano dhidi ya maambukizi ya virusi vya Ukimwi kwa kuelimisha jamii na kuwalinda vijana dhidi ya kila tabia hatarishi inayoweza kusababisha maambukizi ya virusi vya Ukimwi.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge Mhe. Rashid Magope amewashukuru wananchi kwa juhudi zao na uelewa wao juu ya maambukizi ya virusi vya Ukimwi hata kupelekea maambukizi ya virusi vya Ukimwi kupungua kiasi wilayani Sikonge kama takwimu zinavyo onesha mwaka 2023 maambukizi ni asilimia 1.5 ukilinganisha na takwimu za mwaka uliopita 2022 ambapo maambukizi yalikuwa asilimia 1.7.
Naye Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge Bi. Kalista Maina amewasihi wananchi kuendelea kuwa na hofu ya Mungu na kuendelea kuwa waaminifu kwa wale walio katika ndoa ili kujikinga na maambukizi ya virusi vya Ukimwi nchini.
Akiwasilisha Taarifa ya Siku ya Ukimwi Duniani Bi. Haikael Mjema amesema serikali inaendelea na mapambano dhidi ya maambukizi ya Virusi vya Ukimwi na Ukimwi ikiwa ni pamoja na kusaidia kuunda vikundi 42 vya watu wanaoishi na virusi vya ukimwi,Kuendelea kutoa elimu ya ufahamu juu ya matumizi ya sahihi ya dawa za kufubaza makali ya virusi vya Ukimwi,Kuunda klabu tano za Watoto wanaoishi na virusi vya Ukimwi,kuendelea kuwa na vituo ishirini na moja vya kutolea dawa za kupunguza makali ya virusi vya Ukimwi pamoja na Upatikanaji wa dawa za kufubaza makali ya Virusi vya Ukimwi katika vituo vyote vya kutolea huduma sambamba na upatikanaji wa kondomu (mipira ya kiume) kwa mwaka mzima.
Akihitimisha maadhimisho hayo Mhe. Chacha amewashukuru wadau wote walio mstari wa mbele katika mapambano dhidi ya maambukizi ya virusi vya Ukimwi na Ukimwi ikiwa ni pamoja na MDH, IDT, CSSC, NACOPHA na COMPASSION Tanzania.
Mkurugenzi Mtendaji Sikonge DC
Anuani ya Posta: S.L.P 70 Sikonge, Tabora
Simu: 0767135460
Simu: 0767135460
Barua pepe: ded@sikongedc.go.tz
Hatimiliki ©2017Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge, Haki zote zimehifadhiwa