MWENGE WA UHURU WAZINDUA MIRADI YA MAENDELEO WILAYANI SIKONGE.
Na.Anna Kapama.
Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge imepokea Mwenge wa Uhuru mwaka 2021 ukitokea Urambo ambapo Mwenge huo umetembelea miradi mitatu ikijumuisha Sekta ya viwanda, elimu na Maji.
Akiweka jiwe la msingi katika Kiwanda cha kati cha kuchakata na kufungasha mazao ya nyuki Wilayani Sikonge kiongozi wa Mbio maalumu za Mwenge wa Uhuru 2021 Luteni Josephine Mwambashi amepongeza kazi nzuri iliyofanywa na halmashauri hiyo na kuwasisitiza Wasimamizi wa miradi yote inayotekelezwa na serikali kuhakikisha viongozi wa ngazi za chini na jamii kwa ujumla wanashirikishwa ipasavyo ili kujua kinachofanywa na serikali yao.
Kiwanda hicho kimegharimu Sh.Milioni 757.6 katika hatua ya ukamilishaji wa ujenzi wa uzio, mashimo ya maji taka, mnara wa maji, kukamilisha mifumo ya huduma na ununuzi na usimikaji wa mitambo.
Aidha,Luteni Mwambashi amezindua mradi Ofisi za jengo la Uthibiti Ubora wa Elimu ambao umegharimu Sh.Milioni 152.1 na mradi huo umekamilika.Pia amezindua Mradi wa Usambazaji maji katika kijiji cha Kabanga mradi uliogharimu Sh.Milioni 245.3 hadi kukamilika kwake na unawasaidia wananchi wa kijiji cha Kabanga kupata huduma ya maji kwa karibu zaidi.
Miradi yote ina thamani ya jumla ya Shilingi Bilioni 1.2 Kati ya fedha hizo kiasi cha Shilingi Milioni 37.9 ni mchango wa Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge, Shilingi Bilioni 1.1 ni mchango wa Serikali Kuu,huku Wananchi wakichangia Sh. 260,592.0
Mwenge wa Uhuru mwaka 2021 wenye kauli mbiu"TEHAMA NI MSINGI WA TAIFA ENDELEVU ITUMIE KWA USAHIHI NA UWAJIBIKAJI"
Mkurugenzi Mtendaji Sikonge DC
Anuani ya Posta: S.L.P 70 Sikonge, Tabora
Simu: 0767135460
Simu: 0767135460
Barua pepe: ded@sikongedc.go.tz
Hatimiliki ©2017Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge, Haki zote zimehifadhiwa