Na. Robert Magaka – Sikonge.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge Mhe. Rashid Maulid Magope ameongoza baraza la madiwani kwa siku ya pili katika ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri.
Akifungua baraza hilo Mhe. Magope amesema Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge imejipanga kukusanya mapato ya ndani kiasi cha Shilingi Bilioni nne kwa mwaka wa fedha 2023/2024.
Lakini mpaka kufikia tarehe 30 ya Mwezi Septemba 2023, Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge imekusanya kiasi cha Shilingi Bilioni 2.65 ambayo ni sawa na asilimia 65%. “Mwenendo huu wa makusanyo unaridhisha ninaomba wataalam wetu ongezeni jitahada za kukusanya mapato ili tufikie malengo tulio jiwekea” amesema Mhe. Magope.
Kwa upande wa wajumbe wa baraza hilo wamepongeza Taarifa ya ujenzi wa stendi mpya ya mabasi lakini wameomba wapatiwe mchanganuo wa kina wa vifaa vyote vilivyotumika katika mradi huo.
Aidha baraza hilo leo limejikita katika kuboresha ukusanyaji mapato ya Halmashauri,kupokea Taarifa za maendeleo ya kata pamoja na Taarifa za kamati za kudumu za Halmashauri na kuzijadili.
Naye Katibu wa baraza hilo Ndg. Seleman Pandawe akijibu hoja ya Waheshimiwa Madiwani kuhusu namna ya uwasilishwaji wa Taarifa za maendeleo ya kata ufanywe na watendaji wa kata,Ndg. Pandawe amewasihi wajumbe kufuata kanuni,taratibu na sheria za uendeshaji wa Halmashauri na kwa upande wake hayupo tayari kuvunja kanuni hizo bali ameshauri muongozo wa namna ya kuwasilisha Taarifa hizo ufuatwe.
Akifunga Baraza hilo Mhe. Magope amewashukuru wajumbe na wageni waalikwa kwa kuhudhuria baraza hilo na ametoa wito kwa wataalam kuyachukua yale yote yaliyojadiliwa na Kwenda kuyafanyia kazi kwa ajili ya mustakabali wa maendeleo ya Halmashauri.
Mkurugenzi Mtendaji Sikonge DC
Anuani ya Posta: S.L.P 70 Sikonge, Tabora
Simu: 0767135460
Simu: 0767135460
Barua pepe: ded@sikongedc.go.tz
Hatimiliki ©2017Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge, Haki zote zimehifadhiwa