"MWANANCHI DAI RISITI UNAPOCHANGIA MIRADI YA MAENDELEO".DC PALINGO.
Mkuu wa Wilaya ya Sikonge Mhe.John Palingo ameendelea na ziara yake kata ya Pangale akisikiliza kero mbalimbali za wananchi na kuhamasisha ujenzi wa vyumba vya madarasa katika Shule za Msingi zilizopo katika kata hiyo huku akiwaasa wananchi kudai risiti wanapotoa fedha za ujenzi wa vyumba vya madarasa.
Mhe.Palingo ameyasema hayo katika kijiji cha Majengo ambapo amefanya mkutano na wananchi hao na kuongeza kuwa wananchi wanapochangia fedha za maendeleo hasa ujenzi wa vyumba vya madarasa wanapaswa kupewa risiti ili kupunguza mianya ya wizi wa fedha za wananchi lakini pia kuongeza ufanisi kwa watendaji na wasimamizi miradi hiyo.
DC Palingo ameendelea kufanya kampeni ya ujenzi wa vyumba vya madarasa baada ya kubaini kuwa kuna upungufu mkubwa katika Shule za Msingi Wilayani hapo hali inayopelekea wanafunzi kupata elimu katika mazingira yasiyo rafiki kwa kurundikana zaidi ya wanafunzi mia katika darasa moja na matokeo yake baadhi wanafeli mitihani ya kitaifa.
Aidha, Mhe.Palingo ameongeza kuwa ujenzi wa maboma ya vyumba vya madarasa kwa nguvu za wananchi kutairahisishia Serikali kupitia tozo za miamala kutoa fedha zitakazokamilisha ujenzi huo.
Na.Anna Kapama.
Mkurugenzi Mtendaji Sikonge DC
Anuani ya Posta: S.L.P 70 Sikonge, Tabora
Simu: 0767135460
Simu: 0767135460
Barua pepe: ded@sikongedc.go.tz
Hatimiliki ©2017Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge, Haki zote zimehifadhiwa