Msimamizi wa Uchaguzi Wilayaya Sikonge, Ndg. Seleman Pandawe, amekutana na viongozi wa vyama vya siasawilaya ya Sikonge kwa ajili ya kujadili maandalizi ya uchaguzi wa Serikali zaMitaa utakaofanyika tarehe 27 Novemba, 2024. Katika kikao hicho kilichofanyikakatika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri, Ndg. Pandawe amewashukuru viongozihao kwa kuhudhuria na kuwa sehemu ya majadiliano muhimu kwa mustakabali wauchaguzi huo.
Akifungua kikao hicho,Pandawe amewakumbusha viongozi hao juu ya umuhimu wa kuzingatia sheria nakanuni za uchaguzi wakati wa kutekeleza majukumu yao. Amesisitiza kuwa amani nausalama katika mchakato wa uchaguzi yapo mikononi mwao, na hivyo kila kiongozi anajukumu la kuhakikisha uchaguzi unafanyika kwa amani na utulivu.
Katika mada inayohusurushwa, Afisa kutoka ofisi ya Takukuru Wilaya ya Sikonge, Ndg. Salum Makina,ametoa tahadhari kali kuhusu vitendo vya rushwa katika uchaguzi. Ameeleza kuwakutoa au kupokea fedha au kitu chochote kwa mpiga kura ili apige kura kwamanufaa fulani au aache kupiga kura ni kinyume cha sheria na inaweza kusababishamadhara makubwa. Amewahimiza viongozi hao kuepuka vitendo vya rushwa kwa nguvu,ili kuhakikisha uchaguzi wa Serikali za Mitaa unakuwa huru na haki.
Kwa upande wake, Kamanda waJeshi la Polisi Wilaya ya Sikonge, SSP. Prosper Ngowi, ametoa wito kwa viongoziwa vyama vya siasa kuzingatia sheria na kanuni zinazohusu uchaguzi, na kuepukakutumia sheria mkononi. Amesema kuwa endapo kiongozi atapata changamoto yoyote,basi hatua za kisheria zifuate kwa haraka. “Hupaswi kujichukulia sheriamkononi. Ukikosewa, toa taarifa kituo cha polisi. Tuna dawati la uchaguzi palena tutachukua hatua mara moja,” ameeleza Kamanda Ngowi.
Viongozi wa vyama vya siasawameonesha furaha yao kwa kufanyika kwa kikao hicho, wakieleza kuwakimewajengea uwezo na kuwakumbusha wajibu wao katika kuhakikisha uchaguziunafanyika kwa haki. Kiongozi wa chama cha ACT Wazalendo, Ndg. Kulwa JumaFundi, amesema, “Kuna maisha baada ya uchaguzi, tufanye kazi kwa uwazi na haki,naamini hakuna atakayegombana na mtu.”
Akifunga kikao hicho, Ndg.Pandawe ameahidi kutoa ushirikiano wa kutosha kwa viongozi hao na amewatakakutokuwa chanzo cha vurugu na taharuki katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa,amesisitiza umuhimu wa kufanya uchaguzi katika mazingira ya amani.
Mwisho.
Mkurugenzi Mtendaji Sikonge DC
Anuani ya Posta: S.L.P 70 Sikonge, Tabora
Simu: 0767135460
Simu: 0767135460
Barua pepe: ded@sikongedc.go.tz
Hatimiliki ©2017Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge, Haki zote zimehifadhiwa