"MSEMAJI MKUU WA SHUGHULI ZA KIUTENDAJI ZA HALMASHAURI YA SIKONGE NI MKURUGENZI" DHRO KAYANGE.
Mkuu wa Idara ya Utawala na Rasilimali watu (W) Ndg.NICO KAYANGE amewataka watumishi wa Umma Wilaya ya Sikonge kuepuka kuisemea Halmashauri kwa kuwa anaetakiwa kusemea shughuli za kiutendaji katika Halmashauri ni Mkurugenzi Mtendaji.
Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji(W) Ndg.Kayange ametoa kauli hiyo kwa watumishi wa Umma Kata ya Kitunda na Kiloli baada ya kubaini kuwepo kwa baadhi ya watu ambao wamekuwa wakitoa taarifa na takwimu kwa muda usio sahihi na taarifa zisizo sahihi.
"Watumishi epukeni kuwa wasemaji wa taasisi, na hata kama kuna mtu amekuhoji kusemea jambo fulani omba kibali kwa Mkurugenzi..vinginenvyo si ruhusa kufanya hivyo hata kama una taarifa ya jambo hilo wewe sio msemaji wa Halmashauri...zingatieni mipaka ya kazi".. DHRO KAYANGE.
Sambamba na hilo Ndg.Kayange amewasisitiza watumishi wa Umma kutunza nyaraka za serikali kwa kuhifadhi sehemu salama na pia kuepuka kusambaza kwa namna yoyote katika ofisi zisizo za serikali kama steshenari.
Ziara ya Mkurugenzi imeendelea katika kata za Kitunda na Kiloli ambapo Wakuu wa Idara mbalimbali wameongozana na Kaimu Mkurugenzi na kukutana na watumishi wa Idara mbalimbali wa Kata hizo kwa lengo la kuwapa maelekezo na kuwakumbusha kufuata sheria na taratibu za utumishi wa Umma wanapokuwa wakitekeleza majukumu yao huku akiwasililiza changamoto/kero wanazokutana nazo wawapo katika vituo vyao vya kazi.
Na.Anna Kapama
Mkurugenzi Mtendaji Sikonge DC
Anuani ya Posta: S.L.P 70 Sikonge, Tabora
Simu: 0767135460
Simu: 0767135460
Barua pepe: ded@sikongedc.go.tz
Hatimiliki ©2017Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge, Haki zote zimehifadhiwa