ML. 25 KUWAHAMISHA WANAFUNZI KWENYE NYASI.
Katika shule ya msingi Mwamalugu iliyopo kata ya Kirumbi wanafunzi wanasomea kwenye madarasa ya Nyasi jambo ambalo limewafanya wanakijiji kuchanga pesa kwa ajili ya ujenzi wa boma la vyumba vitatu vya madarasa.
Ziara ya kamati ya fedha ilifanywa na madiwani katika Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge Mkoani Tabora wakishirikiana na wataalamu mbalimabi wa Halmashauri hiyo yaibua uwajibikaji wa wananchi katika kuchangia miundombinu ya kimaendeleo.
Miongoni mwa Miradi inayoendeshwa kwa nguvu za wananchi katika Wilaya ya Sikonge.
Mwenyekiti wa Halmashauri(W) Mhe. Peter Nzalalila alikuwa kiongozi wa msafara aliwapongeza wananchi kwa kujitolea nguvu zao pamoja na pesa zao kuchangia ili kushilikiana na serikali ya awamu ya tano katika kuleta maendeleo.
Pia aliwapongeza kwa jambo hilo kwani jamii nzima ina wajibu wa kuhakikisha watoto wote wanapata elimu bora katika mazingira bora yatakayo wavutia kusoma kwa bidii ili kutimiza ndoto zao. Hivyo basi wazazi wazidi kuhimizwa kutosita kuchangia maendeleo mara tu wanapohitajika.
Katika ziara hiyo madiwaani waliahidi kutenga Ml. 25 watakapokaa kwenye baraza la madiwani kwa ajili ya kukamilisha boma hilo la vyumba vitatu vya madarasa ili wanafunzi wanapate madarasa bora ya kusomea na kuondokana na adha ya kusomea kwenye madarasa ya miti yaalioezekewa nyasi.
Jambo hili lilipokelewa kwa mikono miwili na viongozi wa kijiji cha Mwamalugu pamoja na wananchi kwa kuhaidi kuendelea kushiriki kama nguvu kazi huku wakiupongeza uongozi wa awamu ya tano kwa kusema ni uongozi unaoacha alama kwa wananchi wake kwani pamoja na elimu kuwa bure lakini pia serikali imeendelea kuwezesha ujenzi wa vyumba vya madarasa na ofisi za walimu.
Ili kuondoa msongamano wa wanafunzi kwenye chumba kimoja cha darasa ilishauliwa kwa uongozi waa kata husika kuhakikisha kuwa wanamalizia mradi waliouanzisha kwanza kabla ya kuingia kwenye mradi mwingine wa ujenzi wa shule mpya.
Miongoni mwa miradi ya elimu iliyokaguliwa ilikuwa ni pamoja na ujenzi wa shule ya sekondari ipole, kipili, Kirumbi pamoja na Kiwele sekondari inayotegemewa kupokea wanafunzi wa kidato cha tano kwa mwaka 2019 ambayo imekamilika na mabweni yakiwa katika hatua za mwisho za umalizikaji. Yote hii imefanywa na serikali ya awamu ya tano ikiwa katika kutekeleza ilani yake ambapo moja ya kipaumbele ni Elimu.
Mkurugenzi Mtendaji Sikonge DC
Anuani ya Posta: S.L.P 70 Sikonge, Tabora
Simu: 0767135460
Simu: 0767135460
Barua pepe: ded@sikongedc.go.tz
Hatimiliki ©2017Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge, Haki zote zimehifadhiwa