Na Edigar Nkilabo,
Mgenirasmi katika kilele cha Maadhimisho ya Maonesho ya Sikukuu ya WakulimaNanenane, 2025 Mhe.Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Balozi Simon Sirro amewatakawataalamu kuwaelekeza wajasiriamali njia bora ya kutengeneza vifungashiovinavyokidhi vigezo vya kimataifa.
Mhe.Simon Sirro amesema hayo katika Uwanja wa Fatuma Mwasa Ipuli, alipotembeleaBanda la Maonesho la Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge.
"Wataalamuwetu mpo hapa najua mnawatembelea wakulima na kuwapa mbinu nzuri za kuzalishakwa wingi hadi sasa wanafanya kazi nzuri lakini changamoto yao ni vifungashiovya bidhaa wanavyotumia bado havikidhi ubora wa kuwawezesha kupeleka bidhaa zaonje"alisema.
"Jamanimnalipwa na serikali kuwasaidia hawa wakulima,wafugaji na wavuvi ili wazalishekwa tija na kuongeza thamani ya mazao yao hivyo hakikisheni mnawashika mkono nakuwaelimisha ili wazalishe kwa ubora na kuuza nje"aliongeza.
Kwaupande wake Mtaalamu wa Mifugo kutoka Banda la Halmashauri ya Wilaya ya SikongeDkt.Maulid Rajab amesema katika maonesho hayo wataalamu wametoa mafunzo kwawakulima na wafugaji waliotembelea katika banda la Sikonge.
"MheshimiwaMgeni rasmi tumetembelewa na wakulima wengi tumewapa elimu na wakati mwinginetumekuwa tukiwatembelea katika mashamba yao na wamenufaika na ujuzi huo hatakuanza kuzalisha kwa tija"alisema
AidhaDkt.Maulid amesema agizo alilotoa Mgeni rasmi wamelipokea watalifanyia kazi kwakushirikiana na wataalamu wengine ili vifungashio vya bidhaa za wajasiriamaliviwe na ubora stahiki.
Kaulimbiu ya maonesho ya Sikukuu ya Wakulima Nanenane 2025 ni Chagua ViongoziBora kwa Maendeleo Endelevu ya Kilimo,Mifugo na Uvuvi 2025"
Mkurugenzi Mtendaji Sikonge DC
Anuani ya Posta: S.L.P 70 Sikonge, Tabora
Simu: 0767135460
Simu: 0767135460
Barua pepe: ded@sikongedc.go.tz
Hatimiliki ©2017Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge, Haki zote zimehifadhiwa