Mkuu wa mkoa Mhe. Balozi.Dkt. Batilda Buriani ameipongeza halmashauri ya wilaya ya sikonge kwa kupata hati safi kwa mwaka wa fedha 2021/2022. Pamoja na hati safi tuliyoipata zipo hoja muhimu ambazo zinapaswa kufuatiliwa kwa ukaribu, kuhakikiwa na kufungwa.
Pia mkuu wa mkoa ameelekeza kwamba Waheshimiwa Madiwani, Mkurugenzi, Wakuu wa Idara na Vitengo na Watumishi wote kwa pamoja watimize wajibu wao kwa kuzingatia sheria kanuni na taratibu zilizopo. ‘Napenda Kuchukua nafasi hii kulikumbusha Baraza la Madiwani kuhakikisha linawachukulia hatua kali watumishi wote wanaosababisha hoja zinazoleta hasara pasipo upendeleo wala kumuonea mtu yoyote'
Aidha Halmashauri ihakikishe hoja zote zinapatiwa majibu stahiki na kuwasilishwa kwa mkaguzi mkuu wa nje (CEA) kwa ajili ya kuhakikiwa na kufungwa.
Mkurugenzi Mtendaji Sikonge DC
Anuani ya Posta: S.L.P 70 Sikonge, Tabora
Simu: 0767135460
Simu: 0767135460
Barua pepe: ded@sikongedc.go.tz
Hatimiliki ©2017Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge, Haki zote zimehifadhiwa