MKUTANO WA WAFANYABIASHARA - SIKONGE.
EVELINA ODEMBA
HALMASHAURI ya Wilaya ya Sikonge yapongezwa kwa kufanya vizuri katika ukusanyaji wa mapato ambapo mpaka sasa jumla ya Sh. Mil 260 tayari zimekusanywa kati ya Mil. 280 zilizotazamiwa kukusanywa kwa mwaka wa fedha 2018/2019.
Takwimu hiyo ilitolewa na Meneja wa TRA Mkoa wa Tabora Thomas Masese alipokuwa akizungumza katika mkutano na kundi la wafanyabiashara waliopo Sikonge sanjari na kutoa elimu ya kodi ili kuwawezesha kupata uelewa.
Mkutano huo ulioongozwa na mgeni rasmi ambaye alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mhe. Agrey Mwanri uliofanyika Katika ukumbi wa Mwanambuya uliopo Sikonge alisema kuwa wafanyabiashara ni kundi muhimu sana katika nchi hii hivyo wasijione kama Watu ambao wamesahaulika na Serikali yao ndio maana elimu hii ni muhimu kwao kwani itawasaidia kufurahia ulipaji wa kodi kwa maendeleo chanya ya nchi hii.
“hatutaki kuona wafanyabiashara wakiona gari la TRA wanakimbia na kufunga maduka yao, nyie ni watu wa muhimu sana” alisema
Sanjari na elimu hiyo pia wafanyabiashara walipata fulsa ya kutoa changamoto mbalimbali zinazowakwamisha kuendesha biashara ikiwemo utozwaji wa kodi kubwa na faini ambapo Mkuu wa Mkoa aliitaka TRA kuwa na kodi rafiki kwa wafanyabiashara, huku akitoa onyo kuwa hakuna ruhusa ya kufunga biashara ya mtu kwa kigezo cha njia ya kumbana alipe kodi. Vinginevyo njia mbadala zitumike kuwabana wafanyabiashara hao kulipa kodi.
Viongozi mbalimbali katika mkutano wa wafanyabiashara (hawapo pichani) katika ukumbi wa Mwanambuya - Sikonge.
Wakati wa kujibu kero mbalimbali Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge Martha Luleka pia aliwataka wafanyabiashara kuhudhuria vikao vya balaza la madiwani na vikao mbalimbali vinavyoandaliwa na Halmashauri ili kutoa hoja zao mahali hapo ziweze kufanyiwa kazi na sio kukaa na matatizo yao kan akwamba hawana sehemu ya kupata msaada. Sanjari na hayo aliahidi kulifanyia kazi ombi la wafanyabiashara waliohitaji kutengewa eneo kwa ajili ya kuuzia mazao.
Naye Mwenyekiti wa Halmashauri ya Sikonge Mhe. Peter Nzalalila aliongeza kuwa mkutano huo utasaidia kuondoa sintofahamu iliyokuwepo kati ya wafanyabiashara na serikali yao, ndio maana timu imekuja kuwasikiliza na kujua changamoto zinazowakabili Na zitatatuliwa na kuwataka kuchukulia ulipaji wa kodi ni wajibu.
Mkurugenzi Mtendaji Sikonge DC
Anuani ya Posta: S.L.P 70 Sikonge, Tabora
Simu: 0767135460
Simu: 0767135460
Barua pepe: ded@sikongedc.go.tz
Hatimiliki ©2017Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge, Haki zote zimehifadhiwa