Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge Ndg. Seleman Pandawe ameongoza kikao cha kamati ya Lishe kwa kipindi cha robo ya tatu kwa mwaka wa fedha 2023/2024 katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge.
Akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa shughuli za lishe kwa robo ya tatu,Afisa Lishe Wilaya ya Sikonge Bi. Veronica Ferdinand amesema halmashauri ya Wilaya ya Sikonge kupitia divisheni na vitengo mbalimbali imeweza kutekeleza shughuli mbalimbali za lishe kwa ufanisi mkubwa hii ikiwa ni pamoja na utekelezaji wa siku ya afya na lishe ya kijiji pamoja na upandaji wa miche ya miembe 500 katika shule 10 za msingi katika robo hii ya tatu.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge Ndg. Seleman Pandawe amewasihi viongozi katika ngazi mbalimbali kuzingatia kwa makini zoezi la utoaji wa chakula shuleni hasa kwa kuimarisha usimamizi wa zoezi lenyewe hususani ajenda ya kilimo katika shule za msingi na sekondari.
Akifunga kikao hicho Ndg. Pandawe ameagiza watalaam kuongeza juhudi ili kuondoka kabisa katika alama ya njano katika kadi alama ya viashiria vya lishe hasa katika kipengele cha elimu ya lishe ambacho ndio kipengele pekee kilichofanya vibaya kwa kupata asilimia 78.4 ambayo ni njano.
Mkurugenzi Mtendaji Sikonge DC
Anuani ya Posta: S.L.P 70 Sikonge, Tabora
Simu: 0767135460
Simu: 0767135460
Barua pepe: ded@sikongedc.go.tz
Hatimiliki ©2017Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge, Haki zote zimehifadhiwa