MKURUGENZI AKUTANA NA WAFANYA BIASHARA.SIKONGE.
Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge Ndg.Selemani Pandawe amekutana na wafanyabiashara waliopanga katika vibanda vinavyomilikiwa na Halmashauri vilivyo Stendi kuu ya mabasi Sikonge pamoja na Sokoni na kuzungumza nao hasa akiwahamasisha kulipa Kodi ya Serikali ambayo wengi wanadaiwa .
Akizingumza na wafanya Biashara hao Ndg.Pandawe amewataka wote wenye madeni ya muda mrefu kulipa ifikapo Desemba 31, mwaka 2021 ambapo mkataba wao utakuwa umemalizika.Aidha, Mkurugenzi Pandawe ametoa ufafanuzi juu ya tangazo la kupangisha upya vibanda ambavyo wafanya Biashara hao wanamaliza mkataba mwezi huu akisema utaratibu upo kisheria kwamba mkataba unapoisha ni utaratibu sahihi kutoa tangazo ili wenye Sifa na uhitaji wa kupanga waombe ili wapewe vibanda hivyo.
"Kama umelipa Kodi ya Serikali (haudaiwi) na unahitaji kuendelea andika barua ya kuomba mkataba mwingine utapewa kipaumbele"Ndg.Pandawe.
Kwa upande wao wafanya Biashara ambao wanadaiwa wameridhia kulipa madeni yao ya muda mrefu huku wakimuomba Mkurugenzi kuwapa kipaumbele pindi watakapotimiza masharti ya maombi hayo.
Na.Anna Kapama
MKURUGENZI AKUTANA NA WAFANYA BIASHARA.SIKONGE.Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge Ndg.Selemani Pandawe amekutana na wafanyabiashara waliopanga katika vibanda vinavyomilikiwa na Halmashauri vilivyo Stendi kuu ya mabasi Sikonge pamoja na Sokoni na kuzungumza nao hasa akiwahamasisha kulipa Kodi ya Serikali ambayo wengi wanadaiwa .Akizingumza na wafanya Biashara hao Ndg.Pandawe amewataka wote wenye madeni ya muda mrefu kulipa ifikapo Desemba 31, mwaka 2021 ambapo mkataba wao utakuwa umemalizika.Aidha, Mkurugenzi Pandawe ametoa ufafanuzi juu ya tangazo la kupangisha upya vibanda ambavyo wafanya Biashara hao wanamaliza mkataba mwezi huu akisema utaratibu upo kisheria kwamba mkataba unapoisha ni utaratibu sahihi kutoa tangazo ili wenye Sifa na uhitaji wa kupanga waombe ili wapewe vibanda hivyo."Kama umelipa Kodi ya Serikali (haudaiwi) na unahitaji kuendelea andika barua ya kuomba mkataba mwingine utapewa kipaumbele"Ndg.Pandawe.Kwa upande wao wafanya Biashara ambao wanadaiwa wameridhia kulipa madeni yao ya muda mrefu huku wakimuomba Mkurugenzi kuwapa kipaumbele pindi watakapotimiza masharti ya maombi hayo.Na.Anna Kapama
Mkurugenzi Mtendaji Sikonge DC
Anuani ya Posta: S.L.P 70 Sikonge, Tabora
Simu: 0767135460
Simu: 0767135460
Barua pepe: ded@sikongedc.go.tz
Hatimiliki ©2017Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge, Haki zote zimehifadhiwa