MITOWO YALALAMIKIWA NA WAKULIMA.
Chama cha Msingi Mitowo kilichopo wilayani Sikonge mkoani Tabora chalalamikiwa na wakulima wa Tumbaku kwa kutowapatia mikopo ya pembejeo.
Wakizungumzi na mwenyekiti wa Halmashauri ya Sikonge Mhe. Peter Nzalalila wakati alipofanya mkutano wakulima hao walidai kushawishiwa kulima Tumbaku ka wingi huku wakiwa na matarajio ya kukopeshwa Pembejeo lakini matokeo yake hali imekuwa tofauti kwani kati ya wakulima 122 wakulima 89 tu ndio waliokopeshwa pembejeo.
Said Mrisho mwenye namba ya ukulima 287 amesema kuwa wakulima wa Tumbaku Mitowo wamegawanyika katika makundi mawili, kundi liliopata mkopo wa Pembejeo kutoka CRDB na ambao hawajapata mkopo kabisa. Aliomba wakulima ambao hawajakopeshwa wasinyang’we Tumbaku zao kwani wao wametii agizo la waziri mkuu mh. Kassim Majaliwa kuwa mwenye uwezo wa kulima Tumbaku hata hekari 10 alime.
Naye Ally Ramadhani aliupongeza uongozi wa chama cha msingi Mitoo kwa kuwashika mkono ili waendelee kulima ambapo walifanya makisio ya kilo elfu 92. Mifuko 660 ambazo ni sawa na tani 165 na wakulima walikubaliana kugawana eka 2 kila mmoja. Kwa wakulima ambao hawakulima kwa muda mrefu walitakiwa kulima eka moja.
Wakulima wa Tumbaku Mitowo wakisikiliza kwa makini.
Pia waliitaka Bank ya CRDB kuwafikiliwa wakulima wote waliokosa mkopo wa pembejeo ili waweze kuvuna Tumbaku iliyo bora Katika kuchambua wakulima waliokosa mkopo wa pembejeo ni wakulima 11 tu kati ya wakulima 33 walionekana wana sifa za kupata mkopo.
Katika mkutano huo Mhe. Nzalalila aliitaka bodi kuona la kufanya ili kuwasaidiaa hao wakulima walikosa pembejeo kwani wamelima na sifa wanazo. Pia alitoa wito kwa wakulima wote kuandaa mazingira rafiki kwa ajili ya kilimo cha tumbaku ikiwemo majiko Banifu, miti pamoja na kuni ili wakaguzi wanapopita wasiwe na sababu ya kuwanyima mikopo ya pembejeo kwa kigezo cha kukosa sifa.
Alitoa wito kwa Bank inayotoa mikopo kwa wakulima ifanye hivyo kwa wakati na kuzingatia kiwango cha makisio ili kuhepuka tatizo la baadhi ya wakulima wengine kukosa pembejeo, jambo linalosababisha hasara kwa wakulima na kuikosesha serikali mapato katika zao la Tumbaku.
Mkurugenzi Mtendaji Sikonge DC
Anuani ya Posta: S.L.P 70 Sikonge, Tabora
Simu: 0767135460
Simu: 0767135460
Barua pepe: ded@sikongedc.go.tz
Hatimiliki ©2017Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge, Haki zote zimehifadhiwa