Sikonge_Tabora
Na.Anna Kapama
Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhe.Nape Nauye amewaagiza maafisa wasimamizi wa Mitambo ya Kurusha Matangazo ya Redio ya TBC kushughulikia hitilafu ya umeme katika Mitambo ya Kurusha matangazo ya Redio Kwa kuagiza Transfoma kutoka Mwanza Kwa ajili ya kutatua changamoto hiyo ambayo imedumu Kwa takribani Mwezi mmoja na kukosa usikivu wa matangazo hayo Kwa wananchi.
Mh.Waziri Nape ametoa Maelekezo hayo wakati wa ziara ya ukaguzi wa kituo cha kurushia matangazo ya Redio ya TBC Taifa na TBC FM Wilaya ya Sikonge aliyoifanya leo Januari 10, 2022.
Aidha, Mhe.Nauye amewasisitiza wataalamu wa Mitambo hiyo kufunga Teknolojia inayoweza kuzuia radi ili kuondoa changamoto ya Hitilafu ya umeme katika Mitambo ya kurusha Matangazo.
Kwa Upande wake Mbunge wa Jimbo la Sikonge Mhe.Joseph Kakunda ameipongeza Serikali Kwa kuendelea kuboresha Huduma ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano na kuweka minara ambayo imesaidia wananchi wa Wilaya ya Sikonge kupata taarifa mbalimbali za maendeleo kupitia matangazo ya Redio ya TBC.
Usikivu wa Matangazo ya Redio ya TBC Taifa na TBC FM yatarejea Kwa Muda wa Siku saba zijazo mara baada ya Changamoto ya umeme katika Mitambo hiyo kuwa imetatuliwa.
#kaziiendelee
Mkurugenzi Mtendaji Sikonge DC
Anuani ya Posta: S.L.P 70 Sikonge, Tabora
Simu: 0767135460
Simu: 0767135460
Barua pepe: ded@sikongedc.go.tz
Hatimiliki ©2017Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge, Haki zote zimehifadhiwa