MIRADI MIWILI YA MAJI YAZINDULIWA SIKONGE.
Na Anna Kapama
Mkuu wa Wilaya ya Tabora Mhe.Dkt.Yahaya Nawanda amemuwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mhe.Balozi.Dkt.Batilda Buriani katika uzinduzi wa Miradi ya Maji katika Vijiji vya Utimule na Msuva na kuwataka Wananchi kutunza miundombinu ya Maji ili wanaufaike kwa muda mrefu.
Akizungumza na Wananchi wakati wa uzinduzi Mhe.Nawanda amesema Serikali imedhamiria kutoa huduma zote stahiki kwa wananchi ikiwemo huduma ya Maji kwa lengo la kumtua mama ndoo.
Akisoma taarifa ya miradi hiyo Meneja wa RUWASA Mhandisi Fikiri Samadi amesema Miradi yote miwili imegharimu Tsh.Milioni 319.2 kwa Vijiji vya Msuva na Utimule na inahudumia jumla ya watu 2350 Kijiji Cha Msuva na watu 1869 kijijini Utimule.
Kwa Upande wake Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge Mhe.Rashid Magope ameipongeza Serikali kwa kuendelea kutimiza ahadi za utekelezaji wa Miradi mbalimbali ikiwemo ya Maji katika Wilaya ya Sikonge.
Uzinduzi wa Miradi hiyo ya Maji umewapunguzia adha wananchi ambao walikuwa wakitembea umbali mrefu kufata Maji ambapo walikuwa wanatumia muda mrefu na sasa Maji yanapatikana karibu katika maeneo yao.
#kaziiendelee
Mkurugenzi Mtendaji Sikonge DC
Anuani ya Posta: S.L.P 70 Sikonge, Tabora
Simu: 0767135460
Simu: 0767135460
Barua pepe: ded@sikongedc.go.tz
Hatimiliki ©2017Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge, Haki zote zimehifadhiwa