MHIMBILI,BUGANDO ZAHAMIA SIKONGE
Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge, imezindua zoezi la uchunguzi na Tiba kutoka kwa Madaktari Bingwa Nchini leo katika Hospitali teule ya Wilaya CDH iliyopo Kata ya Misheni. Katika uzinduzi huo, Mgeni rasmi, Peres Magiri ambae ni Mkuu wa Wilaya ya Sikonge amesisitiza wananchi kujitokeza kwa wingi ili kupata huduma hii muhimu ambayo inatolewa bure.
Aidha, aliwaasa wananchi kuitumia fursa hii kwa sababu ukiikosa hapa utalazimika kuifuata mbali na kwa gharama kubwa sana. Madaktari hao zaidi ya 30 wamebobea katika fani mbalimbali, wapo mabingwa wa Koo, Pua na Masikio, Mabingwa wa magonjwa ya ndani pamoja na magonjwa ya kina mama na upasuaji mbalimbali.
Pia, Katibu wa CCM Wilaya, Emmanuel Mhene alifurahishwa sana na ujio wa Madaktari hao na kusema “sasa Sikonge inatekeleza Ilani ya chama kwa vitendo.” Zoezi hili la Uchunguzi na Tiba kwa Wananchi wa Sikonge linatekeleza Ilani ya Chama cha Mapinduzi ambacho ndicho kinachoongoza Serikali ya Awamu ya Tano.
Mkurugenzi Mtendaji Sikonge DC
Anuani ya Posta: S.L.P 70 Sikonge, Tabora
Simu: 0767135460
Simu: 0767135460
Barua pepe: ded@sikongedc.go.tz
Hatimiliki ©2017Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge, Haki zote zimehifadhiwa