Aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Sikonge Mhe. Simon Chacha ameaga rasmi leo katika hafla fupi ya makabidhiano ya ofisi yaliyofanyika leo katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge.
Akitoa salamu zake kwa wananchi na viongozi wa Wilaya ya Sikonge Mhe. Chacha amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kumuamini na kumuhamishia wilaya ya Tunduru,ameshukuru kwa ushirikiano aliopewa na wananchi wa Sikonge,Baraza la madiwani,na menejimenti ya Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge.
Naye Mhe. Cornel Magembe amempongeza Mhe. Chacha kwa uongozi wake Sikonge na ameahidi kuendeleza zoezi la kusukuma gurudumu la maendeleo wilayani Sikonge “Kwa hiyo niombe sana uongozi wa halmashauri, tushikamane na kushirikiana.Mimi kama Mkuu wa Wilaya kazi yangu ni kusukuma pale ambapo kuna mashaka ya kwenda na hilo Mhe. Chacha naliweza,kwa kweli niahidi tu kwamba naliweza”amesema DC. Magembe.
Hafla hiyo imehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Halmashauri ya Wilaya ya Wilaya ya Sikonge akiwemo Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Mhe. Anna Chambala, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge Mhe. Rashid Magope,Katibu Tawala Wilaya ya Sikonge Ndg. Andrea Ng'hwani pamoja na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge Ndg. Kelvin Msacky.
Mkurugenzi Mtendaji Sikonge DC
Anuani ya Posta: S.L.P 70 Sikonge, Tabora
Simu: 0767135460
Simu: 0767135460
Barua pepe: ded@sikongedc.go.tz
Hatimiliki ©2017Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge, Haki zote zimehifadhiwa