MHE.KAKUNDA ATEMBELEA MIRADI YA MAENDELEO-SIKONGE.
Mbunge wa Jimbo la Sikonge Mhe.Joseph Kakunda ametembelea miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo ya Afya na Elimu Katika kata ya Tutuo ikiwa ni sehemu ya ziara zake kuangalia miradi ya maendeleo inayotekelezwa katika Wilaya ya Sikonge.
Mhe.Kakunda amewasisitiza Wasimamizi wa miradi ya maendeleo kusimamia kwa juhudi ili iweze kukamilika kwa ubora na kwa wakati hatimaye wananchi wapate huduma stahiki kwa kuwa Serikali ya awamu ya Sita imedhamiria kuwaletea maendeleo wananchi.
Aidha, Mhe.Kakunda ametoa rai kwa wasimamizi watakaozembea na kuchelewesha ukamilishaji wa miradi hiyo kuwa watachukuliwa hatua na kushughulikiwa.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Halmashauri(W), Mhe.Rashid Magope amesisitiza usimamizi thabiti wa vifaa vya ujenzi ili kuepuka mianya ya wizi wa vifaa kwa baadhi ya watu wasio waaminifu .Mhe.Kakunda ameambatana na Mwenyekiti wa Halmashauri ambae pia ni Diwani wa kata ya Tutuo, pamoja Afisa mipango wa Wilaya.
Mkurugenzi Mtendaji Sikonge DC
Anuani ya Posta: S.L.P 70 Sikonge, Tabora
Simu: 0767135460
Simu: 0767135460
Barua pepe: ded@sikongedc.go.tz
Hatimiliki ©2017Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge, Haki zote zimehifadhiwa