Mkuu wa Wilaya ya Sikonge Mhe. Cornel Lucas Magembe ameongoza zoezi la ufunguzi wa mafunzo ya jeshi la akiba kijiji cha urafiki kata ya Usunga wilayani Sikonge.
Akitoa taarifa ya mafunzo hayo Kaimu mshauri wa jeshi la Akiba Wilaya ya Sikonge Ssgt. Dotto Matwili amesema jumla ya vijana 80 wamejitokeza kwa hiyari kushiriki mafunzo hayo adhimu kwa ajili ya ulinzi na usalama wa nchi yetu,mbali na changamoto za baadhi ya vijana kuwa watoro kwa sababu mbalimbali lakini mafunzo hayo yanaendelea vizuri na mpaka siku ya leo ya ufunguzi tayari mafunzo hayo yamefikia asilimia 44 ya utekelezaji wake.Hii ikihusisha masomo ya ujanja wa porini,uzalendo,matumizi ya siraha pamoja na elimu ya kupambana na rushwa.
Akihutubia wananchi waliojitokeza katika hadhara hiyo Mhe. Magembe ametoa wito kwa vijana kushiriki mafunzo hayo kwa wingi,kwani yamebeba fursa nyingi za kiuchumi ikiwa ni pamoja na ajira za kudumisha usalama katika shughuli mbalimbali za kiserikali,ikiwemo mitihani ya kitaifa,ulinzi wa maeneo ya taasisi,usimamizi wa chaguzi mbalimbali pamoja na fursa za kujiunga na majeshi ya ulinzi wa nchi yetu.
Mafunzo hayo yanatarajiwa kufikia tamati mwezi Oktoba mwaka 2024,mafunzo hayo ni kwa mujibu wa sheria za nchi kwa ajili ya kuimarisha usalama,uzalendo na utayari wa kulinda usalama wa nchi yetu Tanzania.
Mkurugenzi Mtendaji Sikonge DC
Anuani ya Posta: S.L.P 70 Sikonge, Tabora
Simu: 0767135460
Simu: 0767135460
Barua pepe: ded@sikongedc.go.tz
Hatimiliki ©2017Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge, Haki zote zimehifadhiwa