Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge Mhe. Rashid Magope ameipongeza Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge kwa kupata hati safi ya ukaguzi wa hesabu za Serikali kwa mwaka wa fedha 2023/2023,ameyasema hayo leo wakati wa kikao cha kawaida cha baraza la madiwani kwa kipindi cha robo ya tatu.
Vilevile baraza hilo limepokea taarifa mbalimbali za kamati za kudumu za halmashauri kwa kipindi cha mwezi Januari hadi Machi 2024,taarifa zilizowasilishwa ni pamoja na kamati ya Fedha,Uongozi na Mipango,Kamati ya Elimu na Afya,Kamati ya Huduma za Uchumi,Ujenzi,Maliasili na Mazingira,Kamati ya UKIMWI pamoja na kamati ya Maadili.
Kwa upande wake katibu Tawala wa Mkoa wa Tabora Dkt. John Mboya amesema watumishi wa umma hawana budi kufuata utawala wa sheria kwa sababu ndio kitu pekee kitakachowahakikishia usalama na amani mahala pa kazi,lakini pia amesisitiza kuvumiliana na kuchukuliana hasa pale mmoja anapokuwa amekiuka taratibu na kanuni za utumishi na sheria ifuate mkondo wake pale tu inapotokea hali isiyovumilika.
Akitoa nasaha zake,Mkuu wa Wilaya ya Sikong Mhe. Cornel Magembe ameliasa baraza na watumishi kuishi kwa kupendana na kuheshimiana kwani bila kusheshimiana kazi haziwezi kufanyika vizuri “Ninaomba mtaalam amuheshimu mwanasiasa ambaye ni diwani lakini mwanasiasa amuheshimu mtaaalam.Ili kazi ziweze kwenda,kwa hiyo hilo ndilo nataka nisisitize sana.”
Akifunga kikao Mhe. Magope naye pia amesisitiza kuheshimiana na kufanya shughuli zote za kiutendaji kwa uwazi na ametoa rai kwa watalaam kupambana ili kukamilisha miradi kabla ya fedha hazijarudishwa hazina.
Mkurugenzi Mtendaji Sikonge DC
Anuani ya Posta: S.L.P 70 Sikonge, Tabora
Simu: 0767135460
Simu: 0767135460
Barua pepe: ded@sikongedc.go.tz
Hatimiliki ©2017Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge, Haki zote zimehifadhiwa