Na. Robert Magaka – Sikonge.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge Mhe. Rashid Magope ameongoza baraza la Waheshimiwa Madiwani la siku ya kwanza la robo ya pili katika Ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge.
Akifungua baraza hilo Mhe. Magope amesema kuwa baraza hili la siku ya kwanza lengo lake ni kupokea taarifa za maendeleo katika kata na kujadili kwa pamoja ili kujua ni nini kimefanyika katika kipindi cha robo hii ya pili.
Naye katibu wa baraza hilo Ndg. Selemani Pandawe amewasihi wajumbe kulinda na kutunza taswira nzuri ya Serikali pamoja na Chama,kwa kuepuka kutuma Taarifa zinazoichafua serikali pamoja na wao wenyewe,bali zipo njia sahihi na salama za kufikisha kero na changamoto zinazojitokeza katika maeneo yao ya utawala na kufanyiwa kazi.
Mhe. Magope amewapongeza wajumbe kwa kazi walizozifanya katika kipindi cha robo ya pili na kipekee ameipongeza kata ya Ipole kwa Kufanya Vizuri katika ukusanyaji wa mapato “Ipole mmefanya vizuri sana,yote kwa yote tunakupongezeni sana,mnazo asilimia zinazotia moyo,mmevuka nusu ya makisio” amesema Mhe. Magope.
Akifunga baraza hilo Mhe. Magope amewataka wajumbe kuzingatia suala la ukusanyaji wa mapato kwani ni kupitia mapato ndipo wanaweza kutekeleza shughuli zao za maendeleo.
Mkurugenzi Mtendaji Sikonge DC
Anuani ya Posta: S.L.P 70 Sikonge, Tabora
Simu: 0767135460
Simu: 0767135460
Barua pepe: ded@sikongedc.go.tz
Hatimiliki ©2017Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge, Haki zote zimehifadhiwa