Na. Edgar Nkilabo - Sikonge.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt.Philip Isdor Mpango ameweka jiwe la Msingi Katika mradi mkubwa wa maji kutoka ziwa victoria wa miji ya Sikonge , Urambo na Kaliua Wenye thamani ya shillingi bilioni 145 ambao unatarajiwa kukamilika mwezi Oktoba , 2025.
Akizungumza katika mradi huo Wilayani Sikonge Dkt.Mpango amewataka wananchi kuutunza mradi huo ili uweze kudumu na kutoa huduma katika miji ishirini na nane itakayofikiwa na mradi huo.
Aidha Dkt.Mpango amesema hizi ni jitihada kubwa za serikali ya awamu ya sita katika kuhakikisha wananchi katika maeneo yote ya nchi wanapata huduma ya maji safi na salama ili kuepukana na matumizi ya maji yasiyo safi na salama ambayo yanayoweza kusababisha magonjwa mbalimbali Kwa wananchi.
Kwa upande wake Naibu Waziri wa Maji Mhandisi KUNDO MATHEW amesema wataendelea kutekeleza miradi yote ya maji kwa wakati na ubora unaendana na thamani ya fedha inayotolewa na serikali huku naye Mbunge wa jimbo la Sikonge JOSEPH KAKUNDA amesema changamoto ya uhaba wa maji safi na salama kwa wakazi wa Sikonge kimekuwa kilio cha muda mrefu na sasa mradi huu utakuwa suluhisho la changamoto hiyo hivyo wananchi wanapaswa kutumia vyema mradi huo kwa kujiletea maendeleo.
Mkurugenzi Mtendaji Sikonge DC
Anuani ya Posta: S.L.P 70 Sikonge, Tabora
Simu: 0767135460
Simu: 0767135460
Barua pepe: ded@sikongedc.go.tz
Hatimiliki ©2017Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge, Haki zote zimehifadhiwa