Mkuu wa Wilaya ya Sikonge Mhe. Simon Chacha ameongoza kikao cha baraza la biashara katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge leo tarehe 10 Septemba,2023.
Akifungua baraza hilo amesema mapato mengi ya Serikali yanatokana na shughuli za watu wanazofanya,hivyo mazingira ya kufanya shughuli hizo yanapaswa kuwa mazingira mazuri ili kuwasaidia wananchi wafanye shughuli zao kwa amani.
Katika baraza hilo wajumbe wamechangia sababu mbalimbali zinazo zorotesha sekta ya biashara,viwanda na uwekezaji ikiwemo utambuaji wa mazingira halisi ya uwekezaji pamoja na kuchelewa kwa kiwanda cha kuchakata mazao ya nyuki kufunguliwa.
Akijibu changamoto hizo Bwana Peter Mpeta Mkuu wa Idara ya Viwanda na Uwekezaji amesema Halmashauri ipo katika hatua za mwisho za kukamilisha ujazwaji wa mkataba na mzabuni Ngoda Traders ili kiwanda kianze uzalishaji rasmi na kwa upande wa maeneo ya uwekezaji Mpeta amesema kuwa maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya uwekezaji hayatabadilishwa hivyo wawekezaji wawe huru kuendelea na uwekezaji hasa katika maeneo ya Stendi Kuu ya Mabasi pamoja na eneo la maegesho ya magari ya mizigo.
Aidha akichangia Mawazo katika eneo la uwekezaji, Katibu Tawala wa Wilaya ya Sikonge Ndg. Andrea Ng’hwani amesema Sikonge bado tunahitaji kuongeza nguvu katika eneo la uwekezaji kwa sababu furasa bado zipo nyingi.
Naye Katibu wa baraza la Biashara Wilaya ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Sikonge Ndg. Selemani Pandawe amesema Sikonge bado ina fursa nyingi katika eneo la uwekezaji hivyo wazawa wasisite kuwekeza kwa nguvu hasa katika Ujenzi wa Shule,Hospitali Pamoja na eneo la Usafirishaji.
Akifunga baraza hilo Mhe. Chacha amewasihi wanachi kulichukulia maanani suala la uwekezaji “ Naomba sana suala la uwekezaji tulizingatie,fursa zipo.Tusiogope kuthubutu,tutafakari,tusichelee kuwekeza Sikonge” amesema DC Chacha.
Mkurugenzi Mtendaji Sikonge DC
Anuani ya Posta: S.L.P 70 Sikonge, Tabora
Simu: 0767135460
Simu: 0767135460
Barua pepe: ded@sikongedc.go.tz
Hatimiliki ©2017Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge, Haki zote zimehifadhiwa