Mkuu wa Wilaya ya Sikonge Mhe. Simon Chacha amezindua zoezi la ugawaji wa vyandarua kwenye kaya katika viwanja vya Tasaf.
Akitoa salamu kwa niaba ya Mkurugenzi wa Bohari ya Dawa,Kaimu Meneja wa TRC Tabora Bw. Adonizedeki Tefurukwa amewashukuru wafadhili hususani Mfuko wa dunia kwa maendeleo kwa kuendelea kutoa mchango wake katika sekta ya afya hasa katika kupambana na Kifua Kikuu,Ukimwi pamoja na Malaria.Vilevile amewaomba wananchi kuzingatia matumizi sahihi ya vyandarua watakavyo gawiwa leo.
Mhe. Chacha akiwahutubia wananchi waliojitokeza kumsikiliza amesema takwimu zinaonesha kuwa Mkoa wa Tabora pamoja na Wilaya ya Sikonge unaongoza kwa maambukizi ya ugonjwa wa malaria hivyo lazima wananchi waelewe kuwa hali ni mbaya na lazima hatua za kupambana na malaria zichukuliwe ikiwa ni pamoja na kufanya usafi katika mazingira yetu pamoja na kuzingatia matumizi sahihi ya vyandarua.
Naye Kaimu Mkuu wa Divisheni ya Afya,Ustawi wa Jamii na Lishe Bi. Grace Mburi amesema hadi sasa Halmashauri imeandikisha kaya 44225 kati ya kaya 56,735 zilizotarajiwa ambayo ni sawa na watu 360,909 kati ya watu 340,409 waliotarajiwa.
Vilevile amesema serikali imejipanga kuangamiza mazalia ya mbu kwa kuhakikisha kila kituo cha afya kinatenga fedha kwa ajili ya kununulia viuadudu kwa mwaka wa fedha ujao hasa katika maeneo sugu yanayotunza mazalia ya mbu.
Akitoa salamu za Halmashauri Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Sikonge Ndugu Seleman Pandawe amewasihi pia wananchi kufanya usafi wa mazingira katika maeneo yao ili kuangamiza mazalia ya mbu waenezao malaria na kutumia chandarua kujikinga na ugonjwa hatari wa malaria.
Zoezi hili linaendelea katika kata zote Wilayani Sikonge kupitia vituo 89 vya kupokelea vyandarua vilivyotengwa.
Mkurugenzi Mtendaji Sikonge DC
Anuani ya Posta: S.L.P 70 Sikonge, Tabora
Simu: 0767135460
Simu: 0767135460
Barua pepe: ded@sikongedc.go.tz
Hatimiliki ©2017Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge, Haki zote zimehifadhiwa