Mkuu wa Wilaya ya Sikonge Mhe. Simon Chacha ameongoza kikao cha kamati ya ushauri Wilaya ya Sikonge kilichofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge.
Akichangia hoja ya uzalishaji katika ngazi ya Wilaya Mhe. Chacha amesema lazima tutumie teknokojia ya kisasa katika uzalishaji wetu ili eneo dogo litoe uzalishaji mkubwa.
Akiwasilisha utekelezaji wa shughuli za maendeleo katika Wilaya ya Sikonge Bi. Mkesika Mageta ambaye ni Afisa Mipango amesema Serikali itaendelea kutoa elimu bila malipo kwa nchi nzima ikiwemo Sikonge.
Wajumbe walio hudhuria kikao hicho wameipokea Taarifa ya utekelezaji wa Shughuli mbalimbali za kisekta kwa moyo mmoja na kushauri kuwa Taarifa ya utekelezaji isisahau kueleza na changamoto pia inazokabiliana nazo katika kutekeleza shughuli za maendeleo.
Akufunga kikao hicho Mhe. Chacha amewataka Wataalam kuboresha Taarifa yao kwa kuongeza kipengele cha changamoto wanazokumbana nazo katika kutekeleza shughuli za maendeleo “Msieleze tu mafanikio muweke wazi na changamoto zinazokabili sekta husika na kwa kupitia kikao hiki wajumbe wataona washaurije ili tusonge mbele” amesema Mhe. Chacha.
Mkurugenzi Mtendaji Sikonge DC
Anuani ya Posta: S.L.P 70 Sikonge, Tabora
Simu: 0767135460
Simu: 0767135460
Barua pepe: ded@sikongedc.go.tz
Hatimiliki ©2017Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge, Haki zote zimehifadhiwa