Na. Robert Magaka – Sikonge.
Akifungua kikao hicho Mkuu wa Wilaya ya Sikonge Mhe. Simon Chacha ametoa wito kwa wananchi kuitikia wito wa kuwapeleka Watoto kwenye vituo vya afya kupata chanjo dhidi ya ugonjwa hatari wa surua na rubella, chanjo hiyo inakusudia kutolewa kwa Watoto wenye umri chini ya miaka mitano mpaka miezi tisa.
Aidha Mkuu wa Divisheni ya Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe Dkt. Christopher Nyalu ameeleza kuwa Chanjo hiyo itatolewa bure ikiwa ni utekelezaji wa kampeni ya Kitaifa ya kupambana na ugonjwa wa surua na rubella nchini.
“Magonjwa haya ya Surua na Rubella hayana tiba mahususi hivyo wataalam hutibu madhara na dalili zake tu,lakini kinga ipo hivyo ni vema wazazi wakaitikia wito wa Serikali wa kuwapatia chanjo Watoto waliolengwa ili kuwakinga na magonjwa haya hatari.Tayari vifaa vya zoezi hili vilishawasili kwa ajili ya kuwahudumia walengwa.
Kulingana na Takwimu za Shirika la Afya Duniani Chanjo ya Surua imeepusha vifo vya Watoto Milioni 56 duniani kote kati ya Mwaka 2000 na Mwaka 2021, kabla ya kugunduliwa kwa chanjo ya Surua 1963, Ugonjwa huu ulikuwa ukiuua Watoto Milioni 2.6 kila mwaka duniani kote.
Akifunga Kikao hicho Mhe. Chacha ametoa wito kwa Wazazi na Walezi kuitikia wito huu wa Serikali wa kuwapatia chanjo Watoto wenye umri chini ya miaka 5 hadi miezi 9 kwani kwa kufanya hivyo watakuwa wameepusha jamii na madhara yanayosababishwa na maradhi haya ya surua na rubella Wilayani Sikonge na Tanzania kwa ujumla.
Mkurugenzi Mtendaji Sikonge DC
Anuani ya Posta: S.L.P 70 Sikonge, Tabora
Simu: 0767135460
Simu: 0767135460
Barua pepe: ded@sikongedc.go.tz
Hatimiliki ©2017Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge, Haki zote zimehifadhiwa