Na. Robert Magaka – Sikonge.
Mkuu wa Wilaya ya Sikonge Mhe. Simon Chacha afungua kikao kazi cha Afisa Elimu Mkoa wa Tabora Ndg. Juma Japhet Kaponda pamoja na Wataalam wa Elimu Wilaya ya Sikonge katika Ukumbi wa Shule ya Sekondari Kamagi.
Akifungua Kikao kazi hicho DC Chacha amempongeza Ndg. Kaponda kwa Uwasilishaji wake mzuri wa maneno ya utangulizi lakini pia amempongeza Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Kiyombo kwa usimamizi mzuri wa Miradi ya ujenzi kwa kuushirikisha umma na kufanya kazi nzuri lakini pia amewapongeza Walimu wa Shule ya Sekondari Kamagi kwa ushirikiano walio nao katika usimamizi wa miradi ya shule.
Aidha amekemea tabia ya baadhi ya Wakuu wa Shule na Walimu Wakuu kutowashirikisha walimu wengine,Viongozi wa eneno husika na jamii katika miradi mbalimbali inayoletwa shuleni,amesisitiza uwazi na uwajibikaji katika usimamizi wa miradi hiyo.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge Mhe. Rashid Magope ameshauri uwepo usawa wa bei katika manunuzi ya vifaa vya ujenzi katika miradi,tofauti na sasa ambapo kumekuwepo na utofauti wa bei ya vifaa vya ujenzi toka shule moja hadi nyingine,ameshukuru pia kwa ujio wa mfumo mpya wa manunuzi (NeST) unaweza kuondoa utofauti huo wa bidhaa moja kuwa na bei tofauti katika eneo moja.
Naye Afisa elimu Mkoa wa Tabora Bw. Kaponda ameshukuru kwa kazi nzuri iliyofanyika mwaka uliopita na kuwaomba walimu kufanya zaidi kwa mwaka wa huu mpya wa masomo.
Kaponda ameongeza kuwa amekuja Sikonge akikusudia kusema na Walimu katika maeneo makuu manne amabayo ni Usimamizi wa Miradi Shuleni,Uandikishaji wa wanafunzi,Mdondoko wa wanafunzi na Mwenendo wa Taaluma Shuleni.
Aidha amesisitiza sana kwa Walimu Wakuu na Wasaidizi,Wakuu wa Shule na Wakuu wasaidizi kujua wajibu walionao katika jamii na Taifa kwa ujumla na kufanya kazi kwa bidi na uadilifu.
Akihitimisha kikao kazi hicho Bw. Kaponda amewasihi walimu kufanya kazi kwa kushirikiana, ubunifu na uadilifu katika majukumu yao ya kila siku.
Mkurugenzi Mtendaji Sikonge DC
Anuani ya Posta: S.L.P 70 Sikonge, Tabora
Simu: 0767135460
Simu: 0767135460
Barua pepe: ded@sikongedc.go.tz
Hatimiliki ©2017Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge, Haki zote zimehifadhiwa