MGOGORO KATI YA WANANCHI NA IDARA YA RASLIMALI ZA MAJI BONDE LA ZIWA TANGANYIKA WAPATIWA UFUMBUZI.
Bwawa la Igigwa,Utyatya-Sikonge.Mkuu wa Wilaya ya Sikonge Mhe.John Palingo ametembelea bwawa la umwagiliaji la Igigwa ambalo ni chanzo cha kilimo cha umwagiliaji Wilayani Sikonge na kutatua mgogoro ulio kuwepo kati ya Idara ya raslimali za maji-Bonde la Ziwa Tanganyika na wananchi ambao wanadaiwa kuendesha shughuli za kibinadamu karibu na chemichemi za bwawa hilo.DC Palingo amekutana na wananchi wa eneo hilo baada ya kupokea malalamiko kutoka kwa wananchi hao kuzuiliwa kufanya Shughuli za kijamii kando ya Bwawa hilo,huku wao wakidai hawakuvunja sheria ya mabwawa kwa kuwa wako umbali wa mita 60 kutoka katika bwawa hilo.Akizungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika kijiji cha Nyakahunga kando ya bwawa hilo DC Palingo amewataka wataalamu hao kutoka Bonde la Mto Tanganyika kupima na kuweka alama kwa kuzingatia sheria za mabwawa .Katika hatua nyingine Mhe.Palingo ametembelea katika Bwawa la Utyatya ambalo ni chanzo kikuu cha upatikani wa maji ya bomba Wilayani Sikonge na kuwataka wanaofanya shughuli za kibinadamu na zinazoashiria uchafuzi wa bwawa hilo kuhama.DC Palingo amewataka wananchi kutunza vyanzo vya maji kwani ni muhimu katika upatikanaji wa maji ya bomba yanayotumiwa na wakazi wengi Wilayani hapo huku akiziagiza mamlaka husika kusimamia sheria pasipo upendeleo kwa wote wanaofanya shughuli za kibinadamu kando kando ya mabwawa hayo kuhakikisha wanahama maeneo hayo huku akimsisitiza diwani wa kata ya Igigwa na watendaji wa kata na vijiji kusimamia utunzaji wa mabwawa hayo ili yadumu kwa muda mrefu.Kwa upande wake Mkuu wa kitengo cha utunzaji vyanzo vya maji-Bonde la ziwa Tanganyika Mhandisi Odemba Cornel amesema waliweka alama(beacon) kwa kuzingatia sheria mbalimbali zinazoruhusu wao kuweka alama zaidi ya mita 60 maeneo ambayo mkondo unaotiririsha maji bwawani unapita.Na.Anna Kapama.
Mkurugenzi Mtendaji Sikonge DC
Anuani ya Posta: S.L.P 70 Sikonge, Tabora
Simu: 0767135460
Simu: 0767135460
Barua pepe: ded@sikongedc.go.tz
Hatimiliki ©2017Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge, Haki zote zimehifadhiwa