Mkuu wa wilaya ya Sikonge Mhe. Cornel Magembe ameongoza zoezi la uzinduzi wa utoaji wa matone ya vitamin A kwa watoto wenye umri chini ya miaka mitano katika hospitali ya Sikonge Misheni ikiwa ni maadhimisho ya mwezi wa afya na lishe kitaifa.
Akihutubia wananchi waliohudhuria tukio hilo ametoa wito kwa wazazi na wananchi wa Sikonge kuitikia kwa wingi kupeleka watoto wote wenye umri chini ya miaka mitano kupata matone ya vitamin A pamoja na dawa za minyoo ili kuwalinda dhidi ya magojwa mbalimbali ambayo yanaweza kuathiri ukuaji wao na wataifa kwa ujumla. “Serikali imeamua kuwekeza fedha nyingi kwa watoto kwa sababu hao ndio taifa la kesho,kwani kuendelea kwa taifa lolote ni lazima wawepo watu wakuliendeleza taifa hilo,bila kuwa na watoto wenye afya njema hakuna taifa la baadaye.”amesema Mhe. Magembe.
Zoezi hilo la utoaji wa matone ya Vitamin A limeenda sambamba na zoezi la upimaji wa hali za lishe kwa watoto wenye umri chini ya miaka mitano. Wilaya ya Sikonge inatarajia kuwapatia matone ya vitamin A watoto 60,676 walio chini ya umri wa miaka mitano ifikapo mwishoni mwa mwezi Juni mwaka 2024.
Mkurugenzi Mtendaji Sikonge DC
Anuani ya Posta: S.L.P 70 Sikonge, Tabora
Simu: 0767135460
Simu: 0767135460
Barua pepe: ded@sikongedc.go.tz
Hatimiliki ©2017Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge, Haki zote zimehifadhiwa