MAGONJWA YASIYOPEWA KIPAUMBELE.
Semina iliyohusisha wajumbe wa kamati ya kupambana na magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele yafanyika Wilayani Sikonge.
Mkuu wa wilaya ya Sikonge Mhe. Peres Magiri ambaye ndiye aliyekuwa mwenyekiti wa semina hiyo kwanza aliupongeza Mradi huo na kusema kuwa una manufaa kwa jamii hivyo kuwataka wajumbe wote kuwa mabarozi.
Hakusita kuizungumzia Wilaya yake kuwa Sikonge yajivunia kufanikisha ugawaji wa dawa kwa asilimia 90% kwa mwaka 2018 ambapo wamefanikisha kwa kiwango kikubwa kuzuia ueneaji wa magonjwa hayo.
Akizungumza na wajumbe mratibu wa mradihuo Mario Venus aliyataja magonjwa hayo kuwa ni Kichocho, Minyoo ya Tumbo, Trakoma, Matende na Mabusha pamoja na Usubi kuwa yamekuwa yakiwapata watu lakini kipindi cha nyuma hayakutiliwa mkazo kama yalivyo magonjwa mengine kama UKIMWI na Kifua kikuu.
Alisema elimu itatolewa kwa jamii ili kurahisisha zoezi la ugawaji dawa jambo lililoungwa mkono na mkuu wa wilaya huku akiongezea kuwa elimu hiyo itolewa hata kupitia Sinema, matukio mbali mbali ya kitaifa ambayo yamekuwa yakiwakutanisha watu kutoka sehemu mbalimbali.
Vile vile aliongeza kuwa magonjwa kama Matende na Mabusha huweza kujificha ndani ya mwili wa binadamu kwa zaidi ya miaka 10 bila kutambulika hivyo basi dawa hizo zilizopangwa kutolewa mwanzoni mwa mwezi Aprili ni muhimu.
IMEANDALIWA NA
KITENGO CHA TEKINOLOJIA HABARI NA MAWASILIANO
(TEHAMA)
SIKONGE.
Mkurugenzi Mtendaji Sikonge DC
Anuani ya Posta: S.L.P 70 Sikonge, Tabora
Simu: 0767135460
Simu: 0767135460
Barua pepe: ded@sikongedc.go.tz
Hatimiliki ©2017Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge, Haki zote zimehifadhiwa