MAENDELEO HAYANA CHAMA
Wananchi waombwa kushiriki kwa nguvu kazi pamoja na malighafi zilizopo kwenye maeneo yao ili kuwezesha miradi ya maendeleo mbali mbali inayotolewa na serikali.
Hayo yalisemwa na Mkuu wa Wilaya ya Sikonge Mhe. Peres Magiri wakati wilipojitolea kuchimba msingi wa jengo la vyumba vitatu vya madarasa katika Shule ya Sekondari ya Kamagi iliyopo kata ya Misheni wilayani hapo.
Mhe. Magiri alishirikiana na viongozi mbalimbali wilayani hapo akiwemo mwenyekiti wa Halmashauri Mhe. Peter Nzalalila, diwani kata ya Sikonge Mhe. Juma Ikombola pamoja na Afisa elimu wa Wilaya ndugu Yusuph Hamza ambaye aliandaa mshikamano huo kwa ajili ya kuhamasisha wananchi kujitolea kwenye ujenzi huo.
Akijibu swali la mwanachi aliyeongelea kuhusu swala la wanasiasa kuingilia kati maendeleo na kupelekea kukwamisha Magiri alisema kuwa “ maendeleo hayana rangi,dini, chama wala ukabila, haya ni yetu sote hivyo ni lazima kila mtu ashiriki” aliongezea kuwa kazi ya kujitolea ni muendelezo na haitoishia kwa siku moja kwani pesa zillizotolewa zisitumike kujenga madarasa matatu tu bali ziongezee madarasa mengine.
Naye Afisa Elimu wa Wilaya ya Sikonge Bwana Yusuph Hamza alisema kuwa kiasi cha Sh. Milioni 60 kimetolewa na serikali kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vitatu vya madarasa hivyo kama wananchi watashiriki nguvu kazi itasaidia kuongeza vyumba.
Mkuu wa wilaya akizungumza na Wananchi wa kata ya Misheni waliojitolea kuchimba Msingi.
Ujenzi huo utasaidia kupokea wanafunzi wa kidato cha tano na sita ambapo mwaka huu itaanza rasmi kwa kupokea wanafunzi 240 wa kidato cha tano. Hivyo kuwa shule ya kwanza Wilayani Sikonge kuwa na wanafunzi wa kidato cha tano.
Mkurugenzi Mtendaji Sikonge DC
Anuani ya Posta: S.L.P 70 Sikonge, Tabora
Simu: 0767135460
Simu: 0767135460
Barua pepe: ded@sikongedc.go.tz
Hatimiliki ©2017Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge, Haki zote zimehifadhiwa