MKURUGENZI MTENDAJI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA SIKONGE AKIFANYA MAZOEZI NA WATUMISHI SIKU YA MWAKA MPYA KATIKA BONANZA LA KUHAMASISHA WANANCHI JUU YA UANZISHAJI WA VIWANDA VIDOGO NA VYA KATI WILAYANI SIKONGE. AIDHA KATIKA BONANZA HILO YALIFANYIKA MASHINDANO MBALIMBALI YA MPIRA WA MIGUU NA MPIRA WA KIKAPU, MGENI RASMI AMBAYE NI KATIBU WA CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM) WILAYA ALIKABIDHI ZAWADI KWA WASHINDI. MPIRA WA MIGUU TIMU YA SIKONGE UNITED ILISHINDA KWA PENATI 5 KWA 4 DHIDI YA HOT STONE, HIVYO SIKONGE UNITED WAKAONDOKA NA ZAWADI YA TSH. 40,000/= HUKU HOT STONE WAKIPATA TSH. 20,000/=
KWA MPIRA WA KIKAPU WA WANAWAKE TIMU YA KURUGENZI ILISHINDA KWA MAGOLI 25 KWA 12 DHIDI YA SIKONGE QUEEN NA HIVYO KUPATA ZAWADI YA TSH. 40,000/= WAKATI SIKONGE QUEEN WAKIPATA TSH. 20,000/=. PIA KWA UPANDE WA AFYA, WANANCHI WALIJITOKEZA KWA WINGI KUCHANGIA DAMU NA KUFANYA VIPIMO MBALIMBALI VYA AFYA ZAO. AMBAPO KIASI CHA DAMU KILICHOPATIKANA NI CHUPA 18 ZA DAMU.
AIDHA, KAIMU MKURUGENZI NDUGU TITO LUCHAGULA ALISOMA HOTUBA ALIYOACHIWA NA MKURUGENZI MTENDAJI BWA. SIMON NGATUNGA JUU YA UANZISHAJI WA VIWANDA VIDOGO KWA KUUNDA VIKUNDI ILI WAPATE MKOPO KUTOKA HALMASHAURI YA WILAYA NA KWA WANAOTAKA KUWEKEZA KATIKA VIWANDA ALISEMA MAENEO YAPO TAYARI YALIYOTENGWA KWA AJILI YA VIWANDA VIKUBWA NA VIDOGO.
MWISHO MGENI RASMI ALIWASHUKURU WANANCHI KWA KUJITOKEZA KWA WINGI KATIKA BONANZA HILO NA KUWATAKA WASHIRIKI KATIKA JAMBO HILI LA VIWANDA AMBALO NDIO KAULI MBIU YA SERIKALI YA AWAMU YA TANO KATIKA KUBORESHA NA KUKUZA UCHUMI WA TANZANIA.
Mkurugenzi Mtendaji Sikonge DC
Anuani ya Posta: S.L.P 70 Sikonge, Tabora
Simu: 0767135460
Simu: 0767135460
Barua pepe: ded@sikongedc.go.tz
Hatimiliki ©2017Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge, Haki zote zimehifadhiwa