Hayo yamesemwa leo katika kikao cha watumishi wa Makao Makuu ya Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge na Mkurugenzi Mtendaji Ndg. Selemani Pandawe alipokuwa akiongea na watumishi hao katika ukumbi wa halmashauri.
Aidha watumishi hao wakiwasilisha kero kwa Mwenyekiti wa kikao hicho ndugu Pandawe,wamelalamikia kutofanyika kwa vikao vya idara na divisheni katika maeneo yao hivyo kuleta sintofahamu ya mambo mengi ambayo kwa kufanyika vikao hivyo yangepatiwa majibu na kupunguza au kuondoa kabisa kero hizo.
Naye Mwenyekiti akijibu juu ya kero hiyo iliyoonekana kuwa ya jumla amesema Wakuu wa Divisheni na Vitengo wanapaswa kukaa vikao na watumishi wao kila mwezi kati ya tarehe 20 hadi 30 na mihtasari ya vikao hivyo iwasilishwe kwa Afisa Utumishi kwa ajili ya ufuatiliaji.
Kwa upande wake Mkuu wa Divisheni ya Utawala na Rasilimali Watu, Ndg. Nico Kayange amesisitiza juu ya watumishi wa umma kuzingatia sheria na kanuni za utumishi hasa katika suala zima la mavazi, kwa kuvaa nguo zenye staha na nadhifu.
Akifunga kikao hicho Ndg. Pandawe amesisitiza watumishi wote kuzingatia sheria kila mtu katika eneo lake lakini pia kutunza siri za serikali wanazopata kuzifahamu kulingana na majukumu yao ya kila siku.
Mkurugenzi Mtendaji Sikonge DC
Anuani ya Posta: S.L.P 70 Sikonge, Tabora
Simu: 0767135460
Simu: 0767135460
Barua pepe: ded@sikongedc.go.tz
Hatimiliki ©2017Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge, Haki zote zimehifadhiwa