KINA BABA NI WASAIDIZI WA WANAWAKE NYUMBANI
Maadhimisho ya Siku ya wanawake Duniani Kiwilaya, yamefanyika katika viwanja vya TASAF, Kata ya Tutuo Wilayani Sikonge. Mgeni Rasmi katika maadhimisho hayo alikuwa ni Mkuu wa Wilaya ya Sikonge, Mhe. Peres Magiri. Ambapo ameongelea suala la wanawake kupewa nafasi katika jamii kwa kuwa wanaweza.
Aidha, akizungumzia ufaulu wa wanafunzi wa kike katika shule, amesema kwa mwaka jana 2017 wasichana waliongoza ukilinganisha na wavulana. Hivyo hawa wasichana walioongoza ni kinamama wa kesho ambao wanaweza kushika nafasi mbalimbali za uongozi na kiutaalamu.
Pia, Mgeni rasmi alielezea ni jinsi gani kinamama wavyofanya kazi kubwa nyumbani ya kulea watoto, kupika na kazi zingine za nyumbani, kazi ambazo mwanamume akiambiwa azifanye hatoweza kuzimudu kwa kiwango anachofanya mwanamke. Aliongeza kwa kusema kuwa “Sisi kina baba ni wasaidizi tu wa wanawake kwa kuwa hatuwezi kuzimudu kazi wanazofanya wanawake kutwa nzima nyumbani…”
“Kuna wanaume hawajali kabisa shughuli zote hizo anazofanya mwanamke nyumbani na wengine bado wanafikia hatua ya kumpiga na hata kumfukuza kwa kosa dogo kabisa ambalo halistahili kutoa adhabu kama hizo” alieleza mgeni rasmi.
Mgeni rasmi aliongelea na kukemea suala la kuwaharibia watoto wa kike masomo kwa kuwapa mimba na wengine kuwaoza wakati bado hawajamaliza masomo yao. Alitolea mfano wa Makamu wa Rais, Mhe. Samia Suluhu kuwa kama asingesoma leo hii asingekuwa katika nafasi hiyo. Alisisitiza na kuwataka wananchi kutoa ushirikiano wa kwa yeyote atakae jihusisha kwa namna moja au nyingine kumharibia mtoto wa kike masomo yake.
Mkurugenzi Mtendaji Sikonge DC
Anuani ya Posta: S.L.P 70 Sikonge, Tabora
Simu: 0767135460
Simu: 0767135460
Barua pepe: ded@sikongedc.go.tz
Hatimiliki ©2017Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge, Haki zote zimehifadhiwa