Na, EDIGAR NKILABO
Mwenyekiti wa Kamati ya Kikao cha Tathimini ya Mkataba wa Lishe kwa Ngazi ya Wilaya amewataka watendaji wote wa kata Wilayani Sikonge kusimamaia na kufuatilia taarifa zote za utekelezaji wa mkataba wa lishe ili kuimarisha hali ya lishe na afya kwa ujumla katika jamii hasa kwa makundi ya watoto wa chini ya miaka 5, kina mama wajawazito, vijana balehe pamoja na wanafunzi wa shule ya awali, msingi na sekondari.
Akizungumza katika kikao hicho katika ukumbi wa Halmashauri kwa niaba ya Mwenyekiti Katibu Tawala wa Wilaya ya Sikonge Andrea Ng’hwani amesema watendaji wa kata wanapaswa kushirikiana na wataalamu wa afya wa Kata na Vijiji ili kupata takwimu sahihi za utekelezaji wa afua za lishe katika maeneo yao hasa upatikanaji wa chakula shuleni.
Kwa upande wake Katibu wa Kikao hicho Ndugu Seleman Pandawe amewataka Watendaji wa Kata kwenda kusimamia uundwaji wa kamati za lishe zinazotokana na wazazi katika shule za msingi na sekondari ili Walimu wabaki na jukumu moja tu, lakufundisha watoto huku wazazi wenyewe wakihakikisha upatikanaji wa chakula.
“Wazazi wakisimamia wenyewe masuala ya chakula itasaidia kupunguza malalamiko ya baadhi ya wazazi kwa Walimu wanaojihusisha na usimamizi wa chakula lakini kama jukumu hilo litabaki kwao basi watajua namna nzuri ya kuhamasisha uchangiaji wa chakula shuleni na ushahidi unaonesha shule zote zenye kamati ya lishe zinafanya vizuri hakuna migogoro.”amesema.
Naye AfisaLishe Wilaya ya Sikonge Bi.Veronica Ferdinand amesema kwa robo ya tatu, Januari hadi Machi 2025 Vijiji vyote 71 vimeweza kutekeleza siku ya Afya na Lishe ya kijiji hii ikiwa na sawa na asilimia 100 ya utekelezaji wake.
Aidha Bi.Veronica amesema kwasasa jumla ya shule 134 kati ya 136 (Msingi na Sekondari) katika Wilaya ya Sikonge zinatoa huduma ya chakula shuleni kwa wanafunzi wa bweni na kutwa huku asilimia 80.1 ya wanafunzi ndio wanaopata chakula wanapokuwa shuleni.
Mkurugenzi Mtendaji Sikonge DC
Anuani ya Posta: S.L.P 70 Sikonge, Tabora
Simu: 0767135460
Simu: 0767135460
Barua pepe: ded@sikongedc.go.tz
Hatimiliki ©2017Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge, Haki zote zimehifadhiwa