Kikao cha Dharura cha Menejimenti ya Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge kimeridhia mpango wa urasimishaji wa miti ya asili leo Novemba 10,2023.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge Bw. Hashim Kazoka akifugua kikao hicho amesema lengo la kikao hicho ni kusikiliza,kujadili na kuridhia mpango wa urasimishaji miti ya asili uendelee ikizingatiwa kuwa Wilaya ya Sikonge ni moja ya Wilaya inayojishughulisha na kilimo cha zao la tumbaku ambalo linachangia sana upotevu wa misitu ya asili inayotokana na uvunaji wa kuni za kuanikia zao la tumbaku.
Akiwasilisha mpango huo mbele ya wataalamu Bw. Zacharia Joseph Mseswa Meneja Msimamizi wa Misitu Endelevu Mkwawa Leaf Tobacco Limited amesema lengo ni kuleta usimamizi shirikishi wa misitu ya asili ya jamii kwa wananchi wenyewe ili kuepusha uharibifu wa mazingira na hatari ya kutokea kwa jangwa.
Naye Mkuu wa Kitengo cha Maliasili na Uhifadhi wa Mazingira Bw. Kelvin Msacky akichangia mpango huo amesema kilimo cha tumbaku kitaendelea lakini uhakika wa misitu yetu ya asili kuendelea upo mashakani hivyo mpango huu ni muhimu kwa uendelevu wa misitu yetu ya asili na utunzaji wa mazingira kwa ujumla.
Akifunga kikao hicho Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Bw. Kazoka amewashukuru wajumbe wote kwa michango yao mizuri pamoja na kuridhia mpango huo.
Mkurugenzi Mtendaji Sikonge DC
Anuani ya Posta: S.L.P 70 Sikonge, Tabora
Simu: 0767135460
Simu: 0767135460
Barua pepe: ded@sikongedc.go.tz
Hatimiliki ©2017Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge, Haki zote zimehifadhiwa