Katibu Tawala wilaya ya Sikonge Ndg. Andrea Ng’hwani kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Sikonge ameongoza kikao kazi cha waganga wa tiba asili na tiba mbadala wilaya ya Sikonge.
Akifungua kikao hicho Ndg. Ng’hwani amesema waganga wa tiba asili imewapasa kuzingatia usafi na afya ya mazingira wanayofanyia kazi,hii ni pamoja na uwepo wa choo, bafu pamoja na malazi salama kwa ajili ya wateja wao.
Vilevile ameongeza kuwa waganga wa tiba ya asili wanapaswa kuzingatia sheria,kanuni na taratibu katika kumiliki zana wanazozitumia katika shughuli zao za kila siku kwa sababu zana hizo nyingi zinatokana na maliasili za nchi kama vile mitishamba,pembe na ngozi za wanyama wa porini.
Mada zilizowasilishwa katika kikao kazi hicho ni pamoja na Ukiukwaji wa maadili ya wizara katika utoaji wa huduma za tiba asili,ushirikishwaji wa tiba asili na wadau wengine na upatikanaji wa vibali toka ofisi ya maliasili na ofisi ya Afisa Utamaduni.
Akitoa salamu za Halmashauri,Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge Bw. Kelvin Msacky ametoa wito kwa waganga wa tiba ya asili wasisite kufika katika ofisi za Halmashauri kwa ajili ya kupata huduma pamoja na ufafanuzi juu ya mambo mbalimbali yanayohusu utaratibu katika eneo lao la tiba za jadi.
Mkurugenzi Mtendaji Sikonge DC
Anuani ya Posta: S.L.P 70 Sikonge, Tabora
Simu: 0767135460
Simu: 0767135460
Barua pepe: ded@sikongedc.go.tz
Hatimiliki ©2017Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge, Haki zote zimehifadhiwa