Kamati ya usalama mkoa wa Tabora ikiongozwa na katibu tawala mkoa Dkt. John Mboya imefanya ziara Sikonge kukagua miradi ya maendeleo itakayopitiwa na mbio za mwenge wa uhuru 2024.
Miradi iliyokaguliwa ni pamoja na ujenzi wa zahanati ya kijiji cha Mkolye,Ujenzi wa barabara ya misheni hadi hospitali ya Moravian Sikonge kwa kiwango cha lami yenye urefu wa mita 550 pamoja na mradi wa uhifadhi wa mazingira katika shule ya sekondari Kamagi.
Kamati ya usalama imeridhishwa kwa kiasi kikubwa na maandalizi yanayoendelea kufanyika wilayani Sikonge na imetoa wito kwa wananchi kujitokeza kwa wingi na kushiriki kikamilifu katika zoezi la kuupokea Mwenge wa uhuru Mkoani Tabora na wilayani Sikonge.
Akihitimisha ziara hiyo Dkt. Mboya amewasihi wananchi wa kijiji cha msuva pamoja na wanafunzi kuzingatia elimu kwa kutoa wito kwa wanafunzi kuacha utoro na ameahidi kwa wanafunzi waliokatisha masomo serikali itahakikisha inawarejesha shuleni. “Wanafunzi kataeni utoro,ambao wameacha shule serikali itawafuata huko huko,bakieni shule kwani taifa linawahitaji.” Ameeleza Dkt. Mboya.
Mwenge wa uhuru 2024,uliobeba kauli mbiu “Tunza mazingira na Shiriki Uchaguzi wa Serikali za Mitaa kwa Ujenzi wa Taifa Endelevu.” unaratajiwa kuwasili mkoani Tabora mnamo Agosti 16,2024 na kukimbizwa wilaya ya Sikonge Agosti 23, 2024.
Mkurugenzi Mtendaji Sikonge DC
Anuani ya Posta: S.L.P 70 Sikonge, Tabora
Simu: 0767135460
Simu: 0767135460
Barua pepe: ded@sikongedc.go.tz
Hatimiliki ©2017Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge, Haki zote zimehifadhiwa