Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Umoja wa Wanawake wa Tanzania (UWT), Bi. Suzan Peter Kunambi ametembelea wilaya ya Sikonge akiambatana na wajumbe wa kamati tendaji katika kutekeleza shughuli mbalimbali za Chama Cha Mapinduzi na kuona utekelezaji wa ilani unavyoendelea wilayani humo.
Bi. Kunambi amempongeza Mkuu wa Wilaya ya Sikonge Mhe. Cornel Magembe pamoja na timu yake ya wataalam wa Halmashauri kwa kuendelea kuchapa kazi kwa ushirikiano mkubwa kati ya chama na Serikali unaoleta tija nzuri katika utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) hasa kupitia fedha za miradi ya maendeleo zinazoletwa na serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan.
“Muendelee kufanya kazi kwa bidii ili wananchi wetu hawa,waendelee kujenga imani zaidi na Chama Cha Mapinduzi na mapenzi yao kwa serikali hii ya awamu ya sita inayoongozwa na mama yetu,mahiri,hodari,jasiri na mchapakazi mama Samia Suluhu Hassan.” Ameeleza Bi. Kunambi.
Akiwa Sikonge atakagua miradi ya maendeleo katika sekta ya elimu na afya na kisha kuhutubia mkutano wa hadhara utakaofanyika katika kata ya Tutuo na baadaye ataelekea mkoani Katavi kuhudhuria wiki ya wazazi kitaifa ambayo inafanyika mkoani humo na kilele chake kitakuwa Julai 13, 2024.
Mkurugenzi Mtendaji Sikonge DC
Anuani ya Posta: S.L.P 70 Sikonge, Tabora
Simu: 0767135460
Simu: 0767135460
Barua pepe: ded@sikongedc.go.tz
Hatimiliki ©2017Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge, Haki zote zimehifadhiwa