KATIBU MKUU UVCCM AKAGUA JENGO LA OFISI ZA HALMASHAURI.SIKONGE.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana CCM Taifa Ndg.Kenani Kihongosi amekagua mradi wa ujenzi wa Jengo la ofisi za Halamashauri ya Wilaya ya Sikonge lenye ghorofa mbili na kumpongeza Mkurugenzi Mtendaji (W) pamoja na wasimamizi wengine kwa kusimamia vyema ujenzi huo ambao unatarajiwa kukamilika kwa sehemu ya ghorofa ya chini ifikapo Disemba 2021.
Akisoma taarifa ya maendeleo ya ujenzi kwa niaba ya Mkurugenzi, Mhandisi Biko Mgeni amesema Halmashauri ilipokea zaidi ya Bilioni 3.18 kutoka Serikali kuu huku Halmashauri ikichangia Tsh.Milioni 718.59 na mpaka sasa ujenzi wa jengo lote umekamilika kwa asilimia 72 huku sehemu ya ghorofa ya chini ikiwa imekamilika kwa asilimia kubwa.
Hata hivyo, Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge imeomba fedha kutoka Serikali kuu kiasi cha Sh.Bilioni 2 ili kukamilisha jengo lote ambalo linakadiriwa kugharimu Tsh.Bilioni 5.7Kukamilika kwa ofisi hizo kutaboresha mazingira yakufanyia kazi kwa watumishi wapatao 159.
Na.Anna Kapama
Mkurugenzi Mtendaji Sikonge DC
Anuani ya Posta: S.L.P 70 Sikonge, Tabora
Simu: 0767135460
Simu: 0767135460
Barua pepe: ded@sikongedc.go.tz
Hatimiliki ©2017Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge, Haki zote zimehifadhiwa