Mkuu wa Wilaya ya Sikonge Mhe. Simon Chacha ameongoza Kamati ya Ulinzi na Usalama Kwenda kukagua maduka ya Wafanyabiashara wa jumla na rejareja Mjini Sikonge kuona hali ya upatikanaji wa Sukari na iwapo wafanyabiashara hao wanauza sukari hiyo kwa kuzingatia bei elekezi ya serikali.
Aidha Mhe. Chacha amewataka wafanyabiashara kuzingatia maagizo ya Serikali ya kuuza sukari kwa mujibu wa bei elekezi inayoaanzia Tsh. 2800/= hadi Tsh. 3000/= ili kuepuka kuwaumiza wananchi.
“Zoezi hili ni la kawaida halilengi kutisha mtu bali lengo ni kuona uwiano wa bei ya sukari mnayouza na ile inayoelekezwa na Serikali”. Amesema Mhe. DC.
Zoezi hili litakuwa endelevu ili kuendelea kuona iwapo maagizo ya Serikali yanafuatwa pamoja na kudhibiti wafanyabiashara wasio waaminifu wanaouza kwa bei zisizo halali na wanaoficha sukari ili iadimike.
Mkurugenzi Mtendaji Sikonge DC
Anuani ya Posta: S.L.P 70 Sikonge, Tabora
Simu: 0767135460
Simu: 0767135460
Barua pepe: ded@sikongedc.go.tz
Hatimiliki ©2017Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge, Haki zote zimehifadhiwa