KAMATI YA SIASA WILAYA YA SIKONGE YARIDHISHWA NA UJENZI WA MIUNDOMBINU YA BARABARA-SIKONGE.
Kamati ya Siasa Wilaya ya Sikonge imefanya ziara ya ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo katika Wilaya hiyo ikiwemo Barabara mbalimbali zinazokarabatiwa na kujengwa na TARURA(W) kwa fedha za Serikali.
Akisoma taarifa ya maendeleo ya matengenezo ya Barabara za makao Makuu ya Wilaya zenye urefu wa KM 0.887, Meneja wa TARURA (W) Mhandisi.Elgidius Method amesema barabara hizo zinazojengwa kwa kiwango cha lami nyepesi zitagharimu Tsh.Milioni 185.57 ikiwa ni fedha kutoka Serikali kuu na zinatarajiwa kukamilika ifikapo Machi 2022.
Sambamba na hilo Kamati hiyo ya Siasa imekagua ukarabati wa Barabara nne za Chabutwa-Magereza,Imalampaka-Usunga, Mwanamkola-Igalula, Chabutwa-Kipanga zinazojengwa kwa kiwango cha ngarawe ambazo zitagharimu Tsh.Milioni 163.56 na zitakamilika ifikapo Mwezi Aprili 2022.Aidha,Kamati hiyo ya Siasa imempongeza Meneja wa TARURA Mhandisi Method kwa kusimamia vyema barabara hizo huku wakitoa rai kwa wananchi kuzitunza barabara hizo ili zidumu kwa mda mrefu.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Sikonge Mhe.Anna Chambala amewataka wasimamizi wa Miradi ya maendeleo kuunga mkono juhudi za Rais Samia Suluhu Hassan kwa kusimamia ipasavyo ili kila fedha inayotolewa na Serikali iendane na thamani ya mradi hatimaye wananchi wanufaike.
Kamati hiyo ya Siasa inaendelea na ziara katika maeneo mbalimbali Wilayani hapo ikikagua utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo.
Na.Anna Kapama
Mkurugenzi Mtendaji Sikonge DC
Anuani ya Posta: S.L.P 70 Sikonge, Tabora
Simu: 0767135460
Simu: 0767135460
Barua pepe: ded@sikongedc.go.tz
Hatimiliki ©2017Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge, Haki zote zimehifadhiwa