Akitoa Taarifa ya utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi (CCM) Mhe. Simon Chacha ameelezea kwa kina juu ya mambo yaliyotekelezwa katika sekta ya Kilimo na Mifugo,Elimu,Miundombinu,Afya,Mazingira,Mawasiliano pamoja na Ulinzi na Usalama.
Mbali na Serikali kuendelea kuwahudumia wananchi kupitia wataalam katika sekta mbalimbali imebainika kuwa bado kuna changamoto zinazokwamisha utekelezaji wa ilani ya Chama cha Mapinduzi kwa ufanisi ikiwa moja ya changamoto hizo ni uhaba wa watumishi katika sekta mbalimbali, hata hivyo Mhe. Chacha ameeleza jinsi Serikali ya Wilaya inavyopambana kuhakikisha changamoto hiyo inakoma,"ipo mikakati ya kuomba kibali cha ajira ili kuweza kuziba pengo hili la uhaba wa watumishi,kuendelea kuwabadilishia kada watumishi waliojiendeleza katika fani zingine" amenena Mhe. Chacha
Aidha Mhe. Joseph George Kakunda,Mbunge wa Jimbo la Sikonge akitoa salamu kwa kamati ya Siasa Wilaya amewaomba wajumbe kuwa tayari kuisadia serikali hasa katika maeneo ambayo miradi ya maendeleo inatekelezwa ikiwa ni kwa kuuunga mkono miradi hiyo na wala sio kukwamisha.
Naye Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Sikonge Mhe. Anna Wilson Chambala amewashukuru wajumbe kwa kupokea na kuridhia Taarifa hiyo,Vilevile ametoa agizo kwa Serikali kuwashirikisha Waheshimiwa madiwani kwa nyaraka katika miradi ya maendeleo inayotekelezwa Katika Wilaya ya Sikonge, “Mradi utambulishwe kwa Vielelezo sio maneno peke yake” amesema Mhe. Chambala.
Mkurugenzi Mtendaji Sikonge DC
Anuani ya Posta: S.L.P 70 Sikonge, Tabora
Simu: 0767135460
Simu: 0767135460
Barua pepe: ded@sikongedc.go.tz
Hatimiliki ©2017Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge, Haki zote zimehifadhiwa