KAMATI YA SIASA MKOA WA TABORA YAFANYA UKAGUZI MIRADI YA MAENDELEO SIKONGE
Na.Anna Kapama-Sikonge DC
Kamati ya siasa mkoa wa Tabora imefanya ziara ya ukaguzi wa miradi ya maendeleo wilayani Sikonge ikiwemo mradi wa ujenzi wa kiwanda cha kati cha uchakataji na usindikaji wa mazao ya Nyuki ,mradi wa ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami na ujenzi wa vyumba vya madarasa,mabweni na bwalo la chakula katika Shule ya Msingi Sikonge Elimu maalumu.
Mwenyekiti wa chama Cha Mapinduzi mkoa wa Tabora, Hassan Mwakasubi ameipongeza Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge kwa kutekeleza ilani ya chama kwa kutekeleza miradi hiyo ya maendeleo ikiwemo ya ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami kutoka Usesula hadi Komanga yenye urefu wa kilomita 108.
Nae mkuu wa mkoa wa Tabora Dkt.Philemoni Sengati amesema mradi huo wa ujenzi wa barabara unaotarajiwa kukamilika mwaka huu utasaidia kukuza uchumi kwa kuongeza mwingiliano wa kibiashara kati ya mkoa wa Tabora na mikoa jirani.
Katika hatua nyingine Kamati ya siasa mkoa wa Tabora ambayo iliongozana na viongozi mbalimbali wa wilaya hiyo akiwemo Mkuu Wilaya ya Sikonge, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Wilaya ya Sikonge na wajumbe wengine wa kamati hiyo waliridhishwa na hatua iliyofikiwa ya ujenzi wa kiwanda hicho cha kati cha uchakataji na usindikaji wa mazao ya nyuki.
Aidha,Mwenyekiti wa CCM mkoa amewataka viongozi na wasimamizi wa mradi huo kusimamia vyema vyama vya wafugaji wa nyuki ili waweze kunufaika na mradi huo,huku Mkuu wa Mkoa wa Tabora akiwaomba watu mbalimbali kutoka maeneo yote Tanzania kuja kuwekeza katika misitu inayopatikana wiliayani hapa.
Kwa upande wake mratibu wa ujenzi wa kiwanda hicho Gadi Mwatebela ameipongeza Serikali ya awamu ya tano kwa kuwapatia fedha kwa ajili ya ujenzi wa kiwanda hicho na kuongeza kuwa kitasaidia kuongeza ajira na kuinua uchumi wa wananchi wa Sikonge na maeneo mengine pamoja na kuongeza pato la taifa na kuwa Kiwanda hicho kilicho katika hatua ya kukamilishwa kitakuwa na uwezo wa kuchakata tani nane kwa siku na tani elfu mbili miamoja na nne, Kwa mwaka.
Katika ukaguzi wa madarasa na bweni la chakula katika shule ya msingi Sikonge elimu malumu,mkuu wa mkoa wa Tabora ameongeza kuwa mradi huo utasaidia utoaji wa elimu bora kwa wanafunzi wenye mahitaji maalumu.
Mandefu Kajuni,ambae ni Mkuu wa Shule hiyo iliyoanzishwa mwa 2011, ameipongeza serikali kwa kuwapatia fedha za kujenga mradi wa bweni,bwalo na vyumba viwiili vya madarasa wenye thamani ya Sh.milioni 220.
Mkurugenzi Mtendaji Sikonge DC
Anuani ya Posta: S.L.P 70 Sikonge, Tabora
Simu: 0767135460
Simu: 0767135460
Barua pepe: ded@sikongedc.go.tz
Hatimiliki ©2017Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge, Haki zote zimehifadhiwa