Kamati ya Lishe ya Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge imeketi leo Novemba 3, 2023 katika kikao cha kawaida cha robo ya kwanza Julai hadi Septemba 2023.
Akifungua kikao hicho Kaimu Katibu Tawala wa Wilaya ya Sikonge Bi. Faraja Hebel ametoa rai kwa Wajumbe kuendelea kutekeleza maagizo ya Serikali kuhusu afua za lishe ambapo Wilaya ikifanya vizuri Mkoa mzima wa Tabora utakuwa umefanya vizuri.
Kwa upande wake Afisa Lishe Wilaya Bi. Veronica Ferdinand akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa kazi za Afya na lishe amesema hali ya unyonyeshaji wa maziwa ya mama pekee ni nzuri kwa asilimia 93% na bado wanaendelea kutoa elimu juu ya unyonyeshaji sahihi na elimu ya lishe katika kata mbalimbali na katika vituo vya afya Wilayani Sikonge.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge Ndg. Seleman Pandawe akichangia mjadala wa Taarifa ya Utekelezaji wa afua za afya wilaya amesisitiza juu ya kusimamia kikamilifu suala la kutoa chakula shuleni kwani kwa kufanya hivyo watakuwa wanatekeleza maagizo ya serikali na kutoa huduma yenye tija kwa wananchi.
Akifunga kikao hicho Mwenyekiti wa kamati hiyo ameagiza watendaji wa kata Kwenda kusimamia na kutekeleza mkataba wa lishe katika maeneo yao kwa ushirikiano mkubwa.
Mkurugenzi Mtendaji Sikonge DC
Anuani ya Posta: S.L.P 70 Sikonge, Tabora
Simu: 0767135460
Simu: 0767135460
Barua pepe: ded@sikongedc.go.tz
Hatimiliki ©2017Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge, Haki zote zimehifadhiwa