Sikonge_Tabora
Kamati ya Fedha Uongozi na Mipango Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge imekagua Miradi 9 ya Maendeleo katika Sekta ya Afya na Elimu
Akizungumza wakati wa ukaguzi huo Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Mhe.Rashid Magope amesema suala la ushirikishwaji wa wananchi na Viongozi wa Ngazi zote za Serikali hasa Vijiji ni Muhimu lizingatiwe ili Wananchi wapate fursa za ajira katika miradi hiyo pamoja na kutambua Serikali inaleta Maendeleo kwa ajili yao.
Kwa Upande wake Diwani wa Kata ya Nyahua Mhe.Andrea Masanja ameipongeza Ofisi ya Mkurugenzi kwa kusimamia vyema Miradi hasa yenye fedha nyingi ikiwemo Jengo la Wagonjwa wa dharura(EMD) huku akiwasisitiza maelekezo ya kuboresha yanayotolewa na Kamati yafanyiwe kazi ili watakapokagua mara nyingine wakute miradi ikiwa katika Ubora zaidi.
Aidha, Mkurugenzi Mtendaji Wilaya Seleman Pandawe ameahidi kuyafanyia kazi maagizo yote yaliyotolewa na Kamati yenye lengo la kuboresha miradi hiyo huku akisisitiza kuendelea kufanya ufuatiliaji kupitia Menejimenti ya wataalamu katika kutekeleza Miradi hiyo kwa ufanisi.
Kamati ya Fedha Uongozi na Mipango imekagua Miradi 9 ikiwemo Jengo la huduma za dharura (EMD) lenye Thamani ya TSH. Milioni 300, Wodi mbili za wanawake na wanaume waliopasuliwa zenye thamani ya Tsh.Milioni 400, Jengo la Kuhifadhia Maiti yenye thamani ya Tsh.Milioni 153, ukarabati wa Maabara ya Sekondari Igigwa Tsh.Milioni 30, Ujenzi wa nyumba ya watumishi TSH.Milioni 90, Matundu ya Vyoo katika Zahanati ya Mole na Igigwa TSH.Milioni 30 ambapo fedha zote ni kutoka Serikali kuu , pamoja na Ujenzi wa Kituo Cha Afya Igigwa Chenye Thamani ya Tsh. Milioni 300.2 fedha za Mapato ya Ndani.
Ziara inaendelea..
#kaziiendelee
Mkurugenzi Mtendaji Sikonge DC
Anuani ya Posta: S.L.P 70 Sikonge, Tabora
Simu: 0767135460
Simu: 0767135460
Barua pepe: ded@sikongedc.go.tz
Hatimiliki ©2017Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge, Haki zote zimehifadhiwa