Kamati ya Fedha Uongozi na Mipango imefanya ziara ya kukagua miradi ya maendeleo katika kata ya Misheni na Chabutwa Wilayani Sikonge.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge Mhe. Rashid Magope ameongoza kamati hiyo kukagua miradi ya ujenzi yenye thamani ya Tsh.838,368,500/= katika kata Misheni na Chabutwa.
Kamati hiyo imepongeza kwa usimamizi mzuri wa miradi ya ujenzi wa Nyumba ya Mkurugenzi uliopo Kata ya Misheni pamoja na ujenzi wa Mabweni na Bwalo la chakula katika shule ya Sekondari Kamagi.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge Ndg. Selemani Pandawe amemsimamisha Uongozi Mkuu wa Shule ya Msingi Matale kupisha uchunguzi kutokana na kushindwa kusimamia vema mradi wa ujenzi katika shule hiyo,lakini pia ameagiza ufanyike ukaguzi maalum wa matumizi ya fedha za mradi huo mara moja.
Naye Diwani wa Kata ya Mole Mhe. Seif Mahanga ametoa rai kwa wananchi kulinda na kutunza majengo ya miradi kwani serikali imetumia fedha nyingi kuleta miradi hiyo ya maendeleo.
Aidha katika majumuisho ya ziara hiyo waheshimiwa wajumbe wa kamati hiyo wameshauri miradi ikamilishwe kwa wakati pamoja na kuondoa dosari ndogondogo zilizoonekana katika baadhi ya miradi iliyokaguliwa.
Kamati hiyo itaendelea na ziara yake kesho katika Kata ya Sikonge na Mkolye.
Mkurugenzi Mtendaji Sikonge DC
Anuani ya Posta: S.L.P 70 Sikonge, Tabora
Simu: 0767135460
Simu: 0767135460
Barua pepe: ded@sikongedc.go.tz
Hatimiliki ©2017Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge, Haki zote zimehifadhiwa