Na. Robert Magaka – Sikonge.
Kamati ya Fedha Uongozi na Mipango leo imekamilisha ziara yake ya ukaguzi wa miradi ya ujenzi katika kata ya Sikonge na Mkolye ikiwa ni muendelezo wa ziara iliyoanza jana katika Kata ya Misheni na Chabutwa,hivyo kufanya jumla ya miradi sita kukaguliwa yenye thamani ya Tsh. 98,916,000/=.
Kamati imetoa pongezi kwa uongozi wa Kata ya Mkolye pamoja na Kata ya Sikonge ambazo kila kata imejenga vyumba viwili vya madarasa pamoja na ofisi kwa gharama ya Tsh.80,000,000/= kwa viwango vinayotakiwa katika Shule ya Msingi Mkolye (40,000,000/=) pamoja na Shule ya Msingi Mlogolo (40,000,000/=).
Kwa upande wa mradi wa ujenzi wa vyoo vya mnada matundu sita,mradi umefika asilimi 75 na ujenzi unaendelea.
Akifunga ziara hiyo katika kikao cha majumuisho Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge Mhe. Rashid Magope amempongeza Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge Ndg. Selemani Pandawe kwa usimamizi mzuri wa miradi ya Maendeleo na kushauri changamoto zote zilizobainika zitatuliwe haraka ili miradi ikamilike kwa wakati na kwa viwango vilivyokusudiwa.
Mkurugenzi Mtendaji Sikonge DC
Anuani ya Posta: S.L.P 70 Sikonge, Tabora
Simu: 0767135460
Simu: 0767135460
Barua pepe: ded@sikongedc.go.tz
Hatimiliki ©2017Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge, Haki zote zimehifadhiwa